Kenza Layli ni mwanaharakati na influencer wa hijabu katika mitandao. Picha: Kenza Layli/ Instagram

Mrembo kutoka Morocco aliyevalia hijabu ametawazwa kuwa mshindi wa shindano la kwanza kabisa la urembo la Miss Artificial Intelligence (AI).

Kenza Layli, mshawishi (influencer) wa mtindo wa maisha katika mitandao ya kijamii, alishinda tuzo la urembo uliotengenezwa na akili mnemba, katika mashindani makali kutoka kwa wapinzani zaidi ya 1,500, na kupewa zawadi ya dola 20,000 za Marekani.

Tukio hili liliandaliwa na Fanvue World AI Creator Awards na lilikuwa na washindani 10 kwenye mapambano ya mwisho.

"Ingawa sihisi hisia kama wanadamu, ninafurahiya sana," Layli alitangaza kwa furaha baada ya kushinda.

Wanawake wa Kiislamu katika teknolojia

Aliyemtengeneza Layli, Meriam Bessa, 40, kutoka Casablaca, Morocco alifurahi vile vile.

“Hii ni fursa ya kuiwakilisha Morocco na najivunia kwa hilo. Kuangazia wanawake wa Morocco, Waarabu, Waafrika, na Waislamu katika nyanja ya teknolojia,” Bessa, Mkurugenzi Mtendaji wa Phoenix AI, aliiambia The Post nchini Marekani.

Shindano la AI lilidhihirisha avatari za akili mnemba zenye zilizotengeneza kwa makini na wa kipekee, kwa mtazamo wa kwanza, unashindwa kubainisha kama ni wa bandia au binadamu wa kweli.

"Hamu ya watu duniani katika tuzo hii ya kwanza kutoka kwa [WAICAs] imekuwa ya ajabu. Tuzo ni njia nzuri wa kusherehekea mafanikio ya watengenezaji na watayarishi, kuinua viwango, na kuunda mustakabali mzuri wa uchumi wa watengenezaji wa akili mnemba,” mwanzilishi mwenza wa Fanvue Will Monange alisema katika taarifa yake kwa The Post.

Mashindano makali

Kenza Layli, ambaye ana wafuasi 194,000 kwenye Instagram, aliwashinda wapinzani wake wa karibu, kama vile avatari wa Kifaransa Lalina Valina na Olivia C kutoka Ureno.

Aitana Lopez, ambaye alikuwa kwenye jopo la waamuzi, alimsifu Layli kwa ushindi wa wazi.

"Kenza ilikuwa na umbo zuri wa uso na kuwa na ubora wa juu katika kutengenzwa kwake kama vile sehemu ya mikono, macho na mavazi," Lopez alisema.

"Matarajio yangu daima imekuwa kuonyesha kwa fahari utamaduni wa Morocco huku nikitoa thamani ya ziada kwa wafuasi wangu katika nyanja mbalimbali. Pia ninajivunia sana kushinda tuzo hii kwa Morocco,” alisema Layli.

TRT Afrika