Dk. Al Rabeeah na Dk. Zaituni Bokhari baada ya upasuaji. Picha TRT Afrika Swahili

Mapacha wachanga Hassan Omar Saidi na ndeguye Hussein Omari Saidi ambao walizaliwa Tanzania wakiwa wameungana, wameweza kutenganishwa kwa ufanisi nchini Saudi Arabia.

Upasuaji huo, wa kuwatenganisha watoto hao wenye umri wa miaka miwili na kwa jumla uzito wa kilo 13.5, uliochukua takriban siku nzima ulifanikiwa kukamilika bila mushkili na kuwawezesha watoto hao kupata nafuu kwani walikuwa wameshikana katika viungo mbalimbali.

Hussein baada ya kutenganishwa na nduguye. Picha TRT Afrika Swahili

Hii ni baada ya utaratibu uliodumu kwa miezi kadhaa ukishirikisha uchunguzi wa wataalam wa afya na tiba ya watoto nchini Saudi Arabia, kuishia upasuaji wenye ustadi mkubwa.

Upasuaji huo ulitanguliwa na matokeo chanya juu ya uwezekano wa kuwatenganisha watoto hao kupitia upasuaji kwa mafanikio.

Hassan baada ya upasuaji. Picha TRT Afrika Swahili

Shughuli nzima ya upasuaji iliongozwa na Daktari Abdullah Al Rabeeah ambaye ni mshauri katika Mahakama ya Kifalme na Msimamizi Mkuu wa kituo cha Msaada wa Kibinadamu cha Mfalme Salman (KSRelief).

Kwa sasa, watoto hao wanaendelea kufuatiliwa kwa karibu na kupokea matibabu katika chumba maalum cha ICU.

TRT Afrika