Shirika la habari la Anadolu (AA), kwa ushirikiano na Shirika la kimatiafa la Maendeleo la Uturuki (TIKA) limetoa mafunzo ya Uandishi wa habari kwa waandishi kutoka mataifa 16 kuhusiana na jinsi na umuhimu wa kuripoti majanga kwa ufanisi.
Mafunzo hayo yaliyotolewa kwenye makao makuu ya shirika la habari la Anadolu mjini Ankara, yakishuhudia ushiriki mkubwa wa waandishi wa habari wa kigeni, akiwemo Yerdana Yerzhanuly, mwandishi maalum na mtangazaji kutoka Shirika la habari la Kazakhstan.
Yerzhanuly alitoa shukrani kwa maarifa muhimu kutoka kwa wanahabari wazoefu wa Anadolu, akihoji kuwa walijifunza vipengele muhimu vya kuzingatia wakati wa kuripoti kutoka maeneo yaliyokumbwa na majanga.
Mafunzo hayo pia yaliangazia ujuzi mpya katika upigaji picha wa majanga, jambo ambalo lilioonekana kuwa la manufaa kwa wanahabari wanaoinukia kama Yerzhanuly.
John Muyamba, mwandishi wa gazeti la New Era nchini Namibia, aliisifu programu hiyo kwa kuwa fursa nzuri ya kuwongeza ujuzi za kuboresha utendaji kazi wao. Muyamba aliongeza kuwa mafunzo hayo yametoa mwongozo muhimu yanayofaa na yasiyofaa kufanywa wakati wa kutoa taarifa kutoka maeneo ya majanga.
Muyamba alisema kuwa pia walijifunza jinsi ya kupiga picha za kuvutia kutoka maeneo ya majanga, na kuongeza mwelekeo mpya katika uwezo wao wa kuripoti.
Akisimulia uzoefu wake katika mafunzo ya Uandishi wa Habari wakati wa matukio yenye maafa kama vile majanga, yaliyowashirikisha waandishi wa habari kutoka ulimwenguni, mwandishi wa mtandao wa televisheni nchini Kroatia Barbara Strbac, kutoka NOVA TV, alieleza changamoto za uandishi wa habari za maafa.
Akichangia uzoefu alioupata baada ya kufika Uturuki kutokana na tetemeko la ardhi lililotokea mnamo Februari 6, Strbac alitoa shukrani kwa usaidizi wa wanahabari wenzake, ambao umerahisisha mambo.
Mwandishi mwingine wa habari kutoka Senegal, Alioune Diouf, alisisitiza umuhimu wa mafunzo hayo, kwa kuzingatia ongezeko la maafa yanayohusiana na mabadiliko ya tabianchi duniani kote.
Diouf alisisitiza umuhimu wa waandishi wa habari kujua jinsi ya kushughulikia majanga, hasa katika mikoa kama Senegal, ambayo mara nyingi huathiriwa na majanga ya asili kama mafuriko.
Mafunzo ya Uandishi wa Habari za Maafa, yaliyofanyika kuanzia Julai 16 hadi 22, yanajumuisha vikao vya mafunzo katika makao makuu ya Anadolu na Urais wa Usimamizi wa Majanga na Dharura (AFAD), pamoja na ziara za ushirika na safari za kitamaduni kwa washiriki.