“Kama tunataka kujilinda na machafuko ya biashara ulimwenguni, hatuwezi kuendelea kuagiza vitu muhimu kama vyakula kwa kiasi kikubwa,” Alisema hayo alipokuwa akizungumza katika kipindi maalum.
Ulikuwa ni wito ambao una athari kwa bara zima la Afrika – Bara la pili duniani kwa wingi wa watu ambapo inakadiriwa kuwa ni makazi ya watu milioni 249 wanaokabiliwa na baa la njaa, kwa mujibu wa makadirio tofauti tofauti. Hiyo ni asilimia 30 ya watu wanaokabiliwa na baa la njaa duniani.
Maombi ya Rais wa Senegal yanaakisi ongezeko la wasiwasi na uharaka kati ya viongozi wa Afrika kuhakikisha usalama wa chakula kwa wananchi wao katika dunia ambayo imekosa uthabiti.
Mwishoni mwa mwezi wa kwanza, wakuu wa nchi, viongozi wa sekta binafsi, wawakilishi wa mashirika ya kimataifa, taasisi zisizo za kiserikali halikadhalika wanasayansi na watafiti walikutana katika mji mkuu wa Senegal, Dakar, kwa mara ya pili kwenye mkutano uliohusu usalama wa chakula.
Kauli mbiu ya mkutano wa pili wa Dakar ulikuwa ni ‘Kuilisha Afrika: uvumilivu na uhuru wa chakula’ – unafanya majumuisho ya changamoto ambayo Afrika inakabiliana nayo wakati dunia ikikabiliwa na hatari ya upungufu wa chakula kutokana na athari za kimazingira na mzozo unaozihusisha Urusi na Ukraine, ambao kwa pamoja ni wazalishaji wakubwa wa ngano duniani.
Na ilikuwa ni Raisi wa Senegal ambaye alitoa msisitizo kwa Afrika kuzalisha chakula kingi zaidi kuliko kutegemea kuagiza kutoka nje pamoja na misaada.
Na mwisho wa mkutano huo wa siku tatu, wadau wa maendeleo waliahidi kuchangia dola bilioni 30 ili kukuza uzalishaji wa chakula barani Afrika ndani ya kipindi cha miaka mitano ijayo, kwa mujibu wa Raisi wa Benki ya maendeleo ya Afrika.
Suala la uhuru wa chakula linabaki kuwa ni moja ya mambo ya msingi kabisa kwa taifa la Senegal. Ikiwa inakadiriwa kuwa asilimia 72 ya kaya zinajihusisha na ulimaji, kilimo kinachukua nafasi muhimu katika uchumi wa nchi.
Lakini nchi hii ya pwani ambayo ipo katika ukanda wa Pwani ya Atlantic, Senegal inaagiza kutoka nje karibu asilimia 70 ya mahitaji yake ya chakula, zaidi ikiwa ni mchele, ngano na mahindi. Utegemezi huu wengi wanashindwa kuuelewa kutokana na nchi hiyo kuwa na nafasi kubwa ya kuweza kujitegemea kwa chakula.
Kwa mfano, bonde la mto Senegal, eneo la River Valley, eneo la kati la kuingilia kati la Delta Land Development Company (SAED), limechukua sehemu muhimu, ikikadiriwa kuwa na ukubwa wa hekari 240,000 zinazofaa kwa umwagiliaji, ambapo ni hekari 121,000 pekee ndizo ambazo kwa saa zimeendelezwa.
Ukiongeza na uwepo wa mtandao mpana wa upatikanaji maji, idadi kubwa ya wafanyakazi na taasisi ambazo zimefumwa kwa ustadi kabisa.
Kwa mujibu wa Aboubacry Sow, Mkurugenzi mtendaji wa SAED, Bonde la Mto Senegal pekee lina uwezo wa kujitosheleza katika uzalishaji wa chakula.
Hata hivyo, hali ilivyo sasa si ya kuvutia kabisa.
Kwa mujibu wa tafiti ya Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), karibu asilimia 16 ya wananchi wa Senegal hawana uhakika wa chakula.
Mwaka 2013, mwaka mmoja baada ya Macky Sall kuchukua nafasi ya urais, Senegal ilikuwa inawekwa namba 154 kati ya nchi 186 kwenye kielelezo cha maendeleo ya binadamu duniani.
Kwa nchi ambayo uchumi wake unategemea zaidi uvuvi, utalii, na uzalishaji wa karanga – ambalo ni zao kuu la biashara kwa Senegal – mapinduzi halisi yalihitajika, hasa katika sekta ya kilimo.
Akiwa anafahamu uwezo mkubwa ambayo nchi yake inayo, Rais wa Senegal ameanzisha mipango kadhaa, ikiwemo mpango wake mkuu, Mpango wa kukuza Kasi ya kilimo - PRACAS II.
Lengo kuu lilikuwa ni kujizalishia mchele wa kutosha ifikapo mwaka 2017. Tarehe ya mwisho iliahirishwa awali mpaka 2019, lakini mpaka kufikia 2023 lengo bado halijafikiwa.
Mtazamo mkubwa zaidi kutoka kwenye mkutano wa Dakar unatoka kwa Akinwumi Adesina, Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika.
“Tunahitaji kuchukua hatua madhubuti sasa ili kujihakikishia upatikanaji wa chakula. Itahitaji mazingira bora zaidi yenye ufanisi, ushindani, utofauti na mfumo wa chakula endelevu. Kilimo lazima kiwe ndio mafuta mapya kwa Afrika.”
Muda wa Afrika kuchukua hatua umeshafika na ni sasa.