Utawala wa Taliban unasema kuwa hautaruhusu mtu yeyote kutishia "uhuru" wa Afghanistan.
Kundi hilo la Taliban liliadhimisha miaka miwili ya kurejea kwao madarakani, siku ya Jumanne ambao wanauita "ushindi wa Kabul," mnamo Agosti 2021. Kurejea kwao kulifuatia mazungumzo ya amani yaliyoendelea miaka mingi na Marekani ambayo yalifanikisha mkataba wa Doha uliotiwa saini Februari 29 mwaka huo.
"Siku hii pia inaonyesha kwamba juhudi zote za wavamizi katika nchi hii zimeshindwa," alisema Zabihullah Mujahid, msemaji wa Taliban ambao wanajitambulisha kama Falme za Kiislamu za Afghanistan yaani IAE.
"Hakuna mvamizi atakayeruhusiwa kutishia utawala na uhuru wa Afghanistan," alisema Mujahid.
"Hawawezi kushinda azimio ya watu Mujahid wa Afghanistan, wala hawawezi kulazimisha utawala wao wa kiholela kwa nguvu na njama," alisema huku akiongeza kuwa utawala wa Taliban "umejitolea kuwatumikia watu wao ndani ya mfumo wa Sharia ya Kiislamu maadamu wangali hai na utafanya kazi kwa maendeleo na utulivu wa nchi."
Aliongeza kuwa utawala wa Taliban "umejitolea kuwatumikia watu wao ndani ya mfumo wa Sharia ya Kiislamu maadamu wangali hai na utafanya kazi kwa maendeleo na utulivu wa nchi."
Chini ya makubaliano ya Doha, majeshi yote ya kigeni yaliihama nchi hiyo iliyokumbwa na vita kufikia mwisho wa Agosti 2021.
Mujahid alisema Umma wote wa Kiislamu - jumuiya ya Kiislamu - "unajivunia" ushindi wa Taliban dhidi ya uvamizi huo.
Msemaji huyo aliongeza kuwa utawala wa Taliban "umehakikisha usalama nchini." "Eneo lote la nchi linasimamiwa chini ya uongozi mmoja, mfumo wa Kiislamu umewekwa na kila kitu kinaelezewa kutoka kwa mtazamo wa Sharia, haya ni matokeo ya kujitolea kwa watu wa Afghanistan kwa miaka mingi," alimaliza.