Tendani alipambana na miaka mingi ya uraibu wa cocaine ambao ulimfanya kupoteza nafasi nyingi za kazi. Picha: Tendani

Katika mazungumzo muhimu ya TED ambayo yanahusiana na mtu yeyote ambaye amepambana na uraibu, mwandishi na mzungumzaji wa Uingereza-Uswisi, Johann Hari, anaelezea wazi kile kinachohitajika ili kuacha kuwa mtumwa wa tabia wa matumizi ya dawa za kulevya.

Katika mazungumzo muhimu ya TED ambayo yanahusiana na mtu yeyote ambaye amepambana na uraibu, mwandishi na mzungumzaji wa Uingereza-Uswisi, Johann Hari, anaelezea wazi kile kinachohitajika ili kuacha kuwa mtumwa wa tabia wa matumizi ya dawa za kulevya.

Hili ni somo la mwanahabari wa Afrika Kusini Tendani Mulaudzi mwenye umri wa miaka 30 ambaye kwa muda mrefu amepitia uraibu wa matumizi ya dawa za kulevya na baadae amejifunza kwa njia ngumu, akipitia mateso ya miaka sita ya uraibu wa cocaine kabla ya kurejesha maisha yake kwenye hali ya kawaida, heshima na kila kitu alichowahi kufanyia kazi.

"Hii ilikuwa mwaka wa 2014, takriban miezi 11 baada ya baba yangu kufariki kutokana na saratani, na nilikuwa nimekunywa pombe kidogo kama njia ya kukabiliana na mawazo," Tendani anasimulia TRT Afrika. "Tulitoka kunywa pombe kwenye klabu kabla ya kuhamia kwa nyumba ya rafiki yangu, ambapo nilipewa cocaine," anasema.

Kilichoanza kama jaribio la kawaida kwenye hafla na marafiki kilimfanya avutiwe haraka na matumizi ya cocaine. Tendani, ambaye wakati huo alikuwa katika mwaka wake wa mwisho katika Chuo Kikuu cha Cape Town, anasema hapo awali alikuwa amejaribu dawa zingine kama kiasi kidogo, lakini hakuwahi kufikiria kuwa angeweza kulewa.

Akiwa na cocaine, mhitimu wa utayarishaji wa vyombo vya habari na filamu alitoka katika kujitambua hadi kuwa mwenye kujiamini ghafla hii ni kutokana na stimu anayoipata baada ya matumizi ya madawa. Lakini kujiamini Huko na shauku ya kuwa na furaha hudumu kwa muda mfupi. Mara tu madawa yanapoisha na ndipo hutamani zaidi na kuongeza kipimo.

Tendani uraibu wake wa matumizi ya cocaine ulikuwa na kuongezeka kutokana na kutumia pesa alizopokea kutoka kwa bima ya maisha ya marehemu babake, na kumaliza pesa hizo ndani ya mwaka mmoja.

"Nilikuwa na umri wa miaka 20 na nilikuwa na kile nilichohisi kama pesa zisizo na kikomo wakati huo; kwa hivyo, nilitoka nje na kuzidiwa na madawa Hayo na hapo ndipo, alipoteza hata elimu yake anakumbuka.

Tatizo lililoenea

Kufuatia kifo cha baba yake, Tendani aligeukia dawa za kulevya ili kukabiliana na hasara hiyo. Picha: Tendani

Tatizo lilioenea baada ya Kilo moja ya cocaine nchini Afrika Kusini kuuzwa kwa dola za Marekani 26,000-29,000 mwaka wa 2022, kulingana na ripoti ya Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC). Ingawa ni kinyume cha sheria, matumizi ya cocaine yameenea.

Ulimwenguni, takriban watu 350,000 hutumia cocaine kila siku, kulingana na data inayopatikana kutoka kwa Mpango wa Kimataifa dhidi ya Uhalifu ulioandaliwa wa Kimataifa. Mbaya zaidi, UNODC inakadiria idadi ya watumiaji wa dawa za kulevya barani Afrika kuongezeka kwa 40% ifikapo 2030.

Kwa upande wa Tendani, elimu ndiyo ilikuwa kipengele kimoja cha kukomboa katika safari yake, na kumweka sawa hata jinsi uraibu ulivyomletea madhara. Licha ya kuongezeka kwa matumizi ya dawa za kulevya, aliendelea na masomo yake ya uandishi wa habari, na kumaliza kati ya wanafunzi watano bora wa kundi lake mnamo 2016.

Uraibu hata hivyo ulimgharimu Tendani kazi kadhaa, na hata uhusiano ambao ulimrudia miaka mingi baada ya kupona. Mnamo 2017, alipewa mafunzo ya kazi katika shirika la habari. Wakubwa wake waligundua kuwa alikuwa mwepesi kazini, na hivi karibuni wakampandisha cheo cha kudumu kama mwandishi wa habari. “Ningeweza kupata taarifa za habari kwa dakika 30, jambo ambalo liliwavutia. Kwa hivyo, nilifanya kazi hiyo kwa takriban mwaka mmoja hadi 2018, wakati mambo yalianza kuwa mabaya," anasimulia.

Mnamo Novemba 2018, alikabiliwa na mhariri wake mkuu wakati huo, ambaye alimuuliza kwa uwazi ikiwa alikuwa na tatizo la matumizi ya dawa za kulevya. "Nilikataa ingawa walikuwa na picha za mimi nikiagiza pombe karibu kila siku."

Tendani aliona aibu sana, hakuja kazini kwa siku tano zilizofuata hadi alipoitwa tena na kuhimizwa kwenda kupata ushauri wa kiafya.

Uraibu kwa mtangulizi

Kunywa pombe kazini ilikuwa mojawapo ya dalili kuu za mapambano ya Tendani na matumizi mabaya ya dawa za kulevya. Picha: Tendani

Hali ya Uraibu inaelezwa kuwa kutokana na Takwimu zilizokusanywa na WHO zinaonyesha kuwa takriban 40% hadi 60% ya watu hurudi tena ndani ya siku 30 baada ya kuondoka kwenye kituo cha matibabu ya dawa na pombe, na hadi 85% wanarudi tena ndani ya mwaka wa kwanza.

Mpango wa matibabu wa wiki tatu ambao Tendani alikuwa amejiandikisha Januari 2019 haukufaulu baada ya kuanza kunywa tena. Kisha alijaribu nyumba ya kuishi kwa kiasi - nyumba inayosimamiwa na watu iliyoundwa kusaidia watu kufanya vitu kwa kiasi - lakini alikamatwa akinywa pombe na kutakiwa kuondoka.

Nchini Afrika Kusini, kupata tiba ya kuondokana na Uraibu wa madawa ya kulevya imeamriwa na mahakama chini ya Sheria ya Kuzuia na Kushughulikia Matumizi Mabaya ya Madawa.

Tishio lililowekwa la urekebishaji ulioagizwa na mahakama hatimaye lilimlazimu Tendani kutafuta suluhu ya muda mrefu kwa tatizo lake la uraibu. "Nilitumia miezi sita katika kituo cha kujiweka sawa na kupona kutokana na uraibu wa madawa cha Healing Wings huko Nelspruit.

Tendani anasema kuangazia kupona husaidia katika kushinda hatari ya kurudi tena. Picha: Tendani

Hapo awali nilisita sana kwenda, lakini niliambiwa kwamba kama nisingeenda kwa kupenda, ningeweza kuamriwa na mahakama na kupelekwa kwenye kituo hicho kwa hadi mwaka mmoja," anaiambia TRT Afrika.

Tendani hakujua kwamba muda wake wa miezi sita ndani ya kituo hicho ungempelekea kuwa mshauri katika kituo hicho hicho. “Nilibadilika sana katika miezi hiyo sita hivi kwamba niliamua kukaa hadi miezi tisa.

Kisha nikaamua kujitolea huko kwa muda wa mwaka mmoja, na hatimaye nikawa mshauri huko.” Pia alianza kuelezea mapambano yake na uraibu kupitia uandishi wa ubunifu - tiba kwa ajili yake mwenyewe na hadithi yake iliyojaa tahadhari kwa wengine. ‘’Nimejifunza jinsi ilivyo muhimu kuweka fikra na kupona,” asema. Tendani alifanya kazi katika Healing Wings kwa karibu miaka miwili hadi 2022, alipoondoka na kurudi kuendelea kutafuta taaluma ya mawasiliano.

Akirejea Johann Hari, hana chochote ila maneno ya kutia moyo kwa wale wanaopambana na uraibu. "Endelea tu kushikamana na mfumo wako wa usaidizi, na usione aibu kuomba usaidizi. Utulivu unaweza isiwe safari rahisi, lakini ni jambo bora zaidi ambalo nimewahi kujifanyia." Anaeleza Tendani.

TRT Afrika