Pete tano za Olimpiki zinaonekana mbele ya mlango wa Jumba la Makumbusho la Louvre huko Paris, Ufaransa - Julai 25, 2024. /Picha: Reuters

Na Tariq Abdul-Wahad

Wiki iliyopita, wanariadha kutoka kote ulimwenguni walifika Paris - mji mkuu wa nchi ambayo mtu anaweza kukosea na kufikiri inaongoza kidemokrasia. Lakini tunajua vizuri zaidi. Tunajua Ufaransa ni taifa kuu la zamani la ukoloni ambalo halina historia nzuri.

Nchi iliyofifia kimaadili ambayo kihalisi ina upungufu wa rasilimali; nchi ambayo inajidanganya kwa kujigamba kwa ukubwa wa "Ufaransa" na kwa hakika ukubwa huo upo tu na si wa kweli. Lakini ni upotovu huu wa ukubwa ndio unaozalisha sera za ubaguzi wa rangi, chuki dhidi ya wageni ambazo nchi inaweka kwa raia wake.

Wanariadha wa Kiislamu wa Ufaransa hawaruhusiwi kuvaa hijabu kichwani wakiwa katika kijiji cha Olimpiki au wakati wa mashindano yao. Kwa nini? Kwa sababu Ufaransa imeshindwa na mradi wake wa kikoloni.

Laiti Ufaransa ingekuwa nchi isiyokua na kiburi, ingetazama ulimwengu wote na ingesikiliza, kutazama na kujifunza. Lakini hata dunia inapoikaribia, Ufaransa inasalia kujiweka peka yake na kuwa na uwezekano wa kupoteza tukio zima.

Akizungumzia kuhusu wanawake wa Kiislamu wa Ufaransa katika riadha, Dk. Haïfi Tlili, mtafiti mwanasosholojia na mwanzilishi mwenza wa kikundi cha wanaharakati wa jamii cha Basket Pour Toutes (Mpira wa Kikapu kwa Wote), alisema, "Wamefichwa na kufanywa kama si binadamu."

Kwa kutumia msimamo mkali wa usekula, jamii ya Wafaransa imekuwa ikiongoza sana katika unyanyapaa. Inatumika kwa madhumuni mawili: kwanza, idadi ya Waislamu inakuwa taa inayotumiwa na wanasiasa kukuza roho yao mpya ya utaifa.

Pili, ni njia kwa watu walionyimwa haki ya kuhisi kama wanashiriki katika mradi wa Ufaransa. "Ikiwa Waarabu na Uislamu wao wana hali mbaya hivi, basi lazima nisiwe chini kabisa. Zaidi ya hayo, ninaweza kuwachukia kila mara."

Sura ya Kweli

Ukweli ni kwamba Ufaransa iko katikati ya mzozo wa kisiasa. Baada ya Rais Emanuel Macron na serikali yake kushindwa katika uchaguzi wa bunge la Ulaya kwa chama cha siasa kali za mrengo wa kulia cha National Rally, Macron alivunja Bunge, jambo ambalo lilianzisha uchaguzi wa wabunge mara moja.

Katika uchaguzi huu, chama cha National Rally kilishinda duru ya kwanza kwa asilimia 33.21. Chama cha National Rally kilishinda katika vituo 25 vya kuhesabu kura na kupata wingi wa viti.

Wiki iliyofuata, Ufaransa ikafichua sura yake ya kweli na kuchukiza ya ubaguzi wa rangi. Wenye kiburi na wanaojiamini wakatoa machamshi ya chukikwenye vyombo vya habari na mitaani kwa ubaguzi wa kila aina usioaminika.

Ushindi wa chama kilichoanzishwa na washirika wa Vita vya Dunia vya pili na wafuasi wa Nazi ulikuwa umekaribia kuchukua uongozi wa Ufaransa. Baadhi ya Wafaransa wasio na asili ya kizungu walishambuliwa kimwili, huku wengine wakihofia mustakabali wao nchini humo.

Maneno yalikuwa zaidi ya sumu. Mtu anaweza kusema ubaguzi wa rangi nchini Ufaransa ulikuwa umefika kileleni.

Katika hali ya kushangaza, mrengo wa kushoto na wa katikati walifanikiwa kuzuia kura za mrengo wa kulia kwa kumwondoa mgombea wao wa tatu katika mchakato wa farasi tatu.

Muungano wa Mrengo wa Kushoto wa Green, Kikomunisti, Socialisti, na "La France Insoumise" uliopewa jina la "Le Nouveau Front Populaire (NFP)" ulishinda viti vingi zaidi katika duru ya pili na kukizuia chama cha mrengo mkali wa kulia kupata ushindi.

Ingawa hatimaye mrengo wa kulia ulishindwa kushinda katika uchaguzi, Macron alionyesha kwamba alikuwa tayari kuhatarisha ustawi wa watu kwa ajili ya malengo yake mwenyewe.

Ufaransa kama taifa kwa muda mrefu imekuwa ikijivunia kuwahudumia wananchi wake. Emmanuel Macron akiwa kwenye usukani wa meli hiyo, imekuwa wazi kuwa maendeleo yoyote ambayo Ufaransa imefanya kuelekea kujiimarisha kama nchi ya demokrasia yameporomoka.

Kubadilisha msimamo mara kwa mara

Hivi majuzi, matumizi ya sehemu ya tatu ya kifungu cha 49 ya katiba ya Ufaransa imekosolewa na kusababisha maandamano, na hata ghasia kwenye makazi ya Macron, na hivyo ndivyo ilivyopaswa kuwa.

Kifungu hiki kinaruhusu serikali kukwepa bunge na kulazimisha kupitishwa kwa sheria, bila kuhitajika upigaji wa kura.

Kwa kutumia hatua zenye utata kama hizi (kupitisha sheria ya kuahirisha umri wa kustaafu), Macron anatupa mtazamo wa kutisha katika akili ya ndani ya serikali aliyoianzisha: utawala ambao unatanguliza umuhimu wa kisiasa na utekelezaji wa haraka wa mageuzi ambayo hayakupendwa na watu wengi, kuliko hata njia ya kidemokrasia na makubaliano ya wananchi.

Baada ya chama cha Macron kushindwa katika Uchaguzi mdogo wa Wabunge wa Ulaya, hakulazimika kulivunja Bunge.

Wengine wanahoji kuwa hatua hiyo ilifanywa ili kuepusha kushindwa wazi wazi; kuvunjwa huko kwa bunge kungezuia vyombo vya habari kuchambua kushindwa huko. Hata hivyo baada ya kuvunjwa huku, alipata hasara nyingine kwa ushindi wa muungano wa mrengo wa kushoto.

Chama chake kilipoteza viti 84 katika mchakato huo. Walakini, alipinga, akidai kwamba mrengo wa kushoto unahitaji kuwa na uwingi kuunda serikali. Uwingi ambao chama chake cha mrengo wa kati haikuwa nayo 2022 alipomteua waziri mkuu mpya.

Tamaa hii ya kushinda kila wakati inamfanya Macron kubadilisha msimamo kila wakati kwa maslahi yake. Tatizo hapa ni mtu hachezi na matakwa ya watu.

Ni mchezo hatari kuucheza katika nchi ambayo utawala wa kiholela tayari umesababisha mapinduzi makali.

Na watu wataasi, haijalishi serikali itachagua kwa jeuri kiasi gani kuwakandamiza wanaopigania haki.

Tumeona haya mara kwa mara kupitia kupigwa marufuku kwa mikutano na maandamano yanayoiunga mkono Palestina katika mji mkuu wa Ufaransa.

Lakini ukweli wa ukoloni umefichuka; watu hawatanyamazishwa tena wala kudanganywa na watawala.

Michezo ya Olimpiki ni ushuhuda wa ukweli huu, huku wanariadha na wafuasi wakibeba bendera za Palestina kama kitendo cha uungaji mkono wa kadhia hio, wakiwemo waogeleaji wa Olimpiki Valerie Tarazi na Yazan al-Bawwab.

Vijana hawa ndio bado wanaheshimu sifa ya taifa hili: Liberté, Égalité, Fraternité. Wana na mabinti wote ambao wabingwa tawala wa Ufaransa wanapigana nao - wale ambao wamenyimwa haki, waliotengwa na kulengwa kwa kweli, ndio walio na vifaa bora zaidi vya kukabiliana na ulimwengu huu mpya. Naomba wafanikiwe.

Mwandishi, Tariq Abdul-Wahad alizaliwa Olivier Saint-Jean nchini Ufaransa mwaka 1974. Alikuwa mchezaji wa kwanza wa mpira wa vikapu wa Ufaransa kuandaliwa na kucheza NBA mwaka 1997. Abdul-Wahid alisoma Historia ya Sanaa katika Chuo Kikuu cha Jimbo la San Jose, na pia ana Shahada ya Uzamili katika Usimamizi wa Michezo.

Kanusho: Maoni yaliyotolewa na mwandishi hayawakilishi lazima maoni, mitazamo na sera za uhariri za TRT Afrika.

TRT Afrika