Ufaransa imemkamata na kumshtaki afisa wa zamani wa ngazi ya juu wa Rwanda kuhusiana na mauaji ya kimbari Rwanda 1994, chanzo kilicho karibu na kesi hiyo kimesema.
Taarifa kutoka chanzo kilichoomba kutotajwa, zinasema kuwa Pierre Kayondo, ambaye alikuwa mkuu wa Mkoa wa Kibuye na pia mbunge wa zamani, alikamatwa Jumanne wiki hii na kushtakiwa kwa kushiriki katika mauaji ya kimbari na uhalifu dhidi ya binadamu, na kuongeza kuwa alikuwa amewekwa kizuizini.
Kayondo alikuwa akisakwa na uchunguzi nchini Ufaransa tangu 2021 baada ya malalamiko kuwasilishwa dhidi yake na mojawapo ya vyama vya waathirika.
Katika malalamiko yao, Kundi la Vyama Vya Kiraia la Rwanda (CPCR) lilimshtaki Kayondo kwa kushiriki kushiriki mauaji na kusaidia kuanzisha makundi yaliyojihami.
Mwanzilishi mwenza wa CPCR Alain Gauthier alielezea kuridhika kwamba "Malalamiko hayo yalifuatiwa na ufunguzi wa uchunguzi na kwamba haki ilimfuatilia Bwana Kayondo. Ni nzuri."
Aliaminika kuishi katika mji wa Bandari ulioko Kaskazini, Le Havre.
Mahusiano ya nchi mbili
Ufaransa imekuwa mojawapo ya maeneo yaliyopendelewa na wahusika wa mauaji wanaokimbia haki juu ya mauaji yaliyowaangamiza takriban watu 800,000, wengi wao wakiwa ni wa kabila la Watutsi, kwa zaidi ya siku 100.
Rwanda, chini ya uongozi wa Rais Paul Kagame, imeishutumu Paris mara kwa mara kwa kutofanya vya kutosha kuwafikisha mahakamani watuhumiwa na pia kutokuwa tayari kuwakabidhi watuhumiwa kwa Rwanda.
Ripoti ya Awali iliyoandaliwa na serikali ya Rwanda ilihitimisha kwamba serikali ya Ufaransa ilikuwa na wajibu "muhimu" wa "kuzuia mauaji ya jamii nzima yaliyoonekana."
Lakini uhusiano kati ya nchi hizo mbili umeimarika tangu ripoti ya wanahistoria iliyoamriwa na rais Emmanuel Macron na kuzinduliwa mnamo 2021 kutambua majukumu "makubwa" ya Ufaransa kwa kushindwa kukomesha mauaji hayo.