Nchini Afrika Kusini na maeneo mengine, wanawake wa vijijini husindika matunda ya mbuyu kwa njia mbalimbali kwa ajili ya chakula. Picha: Reuters

Mbuyu ni mti wa ajabu unaostawi katika mazingira ya mijini, vijijini na misituni. Unaewza kukua kwa upana mkubwa sana na urefu pia na ni miongoni mwa miti inayoishi muda mrefu zaidi duniani.

Kutokana na hadithi zinazohusu mbuyu, muundo wake na hata misemo mbalimbali imefanya mti huu kuongelewa sana na kufanyiwa marejeo mbali mbali ya kibaiolojia mara kwa mara.

Iwapo urembo na ustadi pamoja na miujiza na manufaa zingetiwa katika nyungu moja, basi matokeo yake yangekuwa mbuyu. Unabeba sifa zote, bila kusahau imani za jadi za Kiafrika.

Mbuyu ni mti ambao mara nyingi huwa ni wastani hadi mkubwa kiumbo unaopatikana sehemu nyingi sana Afrika na Australia, unaostawi katika alama sehemu zenye hali ya hewa mbalimbali.

Mti wa Mbuyu unaweza kupewa sifa ya 'mti wa uzima' kumaanisha mti unaoishi na kustawi muda mrefu sana na kutanua na kuenea katika maeneo yote ya anthopolojia ya Afrika ikizungukwa na kil aaina ya itikadi pamoja na maajabu ya kisayansi.

Kulingana na azimio la Umoja wa Mataifa la kupambana na Kuenea kwa Jangwa, mti wa mbuyu “unaweza kuishi hadi miaka 3,000, kukua upana wa hadi mita 50, na kufikia hadi mita 30 kwa urefu.”

Kutokana na utofauti wa kijenetiki kuna takribani aina tisa za mbuyu, sita kati ya hizo hupatikana katika kisiwa cha Madagaska, Mbuyu bado umeendelea kuwa mti usioleweka kutokana na usiri wake.

Miongoni mwa vivutio vya ulimwengu ni mti wa mbuyu wenye asili na wa kuvutia ujulikanao kama Mbuyu wa Sagole unaopatikana nchini Afrika Kusini, ambao kutokana na upekee wake hadi sasa unamiliki rekodi ya dunia ya Guinness.

Senegal ni mojawapo ya nchi za Kiafrika zilizobarikiwa kuwa na miti ya mbuyu ambapo wanawake husindika mbegu na unga. Picha: Reuters

Mbuyu huitwa Kuka kwa lugha ya Kihausa, Reniala kwa Kimalagasi, Mbuyu kwa Kiswahili, Gouye gui kwa Kiwolof, na Zelo kwa Kilingala.

Katika utamaduni wa pop, mbuyu pia hufahamika kama mti ulioota juu chini kwa sababu unaonekana kana kwamba mizizi yake inamea juu angani.

Jina lingine, lisilojulikana sana, ni “krimu ya mti wa Tartar” – rejeleo la ganda la mbuyu, ambalo majimaji yake yana asidi ya citric ya kutosha kutumika kugandisha maziwa, na pia kutumika katika kupikia, kuoka na kutengeneza kileo.

Kutoweka polepole kwa mti wa Mibuyu

Mbuyu ni mti wa ajabu unaostawi katika mazingira ya mijini, vijijini na misituni. Ni miongoni mwa miti mikubwa inayoishi muda mrefu zaidi duniani.

Kuanzia Madagaska, Afrika Kusini na Zimbabwe hadi Senegal, DRC na Nigeria, misitu yenye kupendeza ya mbuyu hupamba mandhari ya Afrika.

Kisayansi, licha ya mbao yake laini, mbuyu umethibitishwa kuwa mti sugu unaohimili moto. “Isipokuwa imekaushwa vizuri, mbao za mbuyu hazichomeki zinapowashwa moto,'' Dkt. Mustapha Karkarna, mtaalam wa usimamizi wa misitu katika Chuo Kikuu cha Bayero cha Nigeria Kano, ameiambia TRT Afrika.

Kuwepo kwa mbuyu ni ushuhuda tosha kwenye ikolojia ya makazi ya binadamu, pia mti huu umekuwa na matumizi mengi kama vile umetumika kama dawa na kwenye ufundi wa kutengeneza samani.

Majani ya mbuyu hutumiwa kama viungo vya chakula ama mbichi au kavu. Picha AFP

''Kiikolojia, ni muhimu sana ndio maana ni nadra sana kwa watu kuukata mtu huu.'' anasema. ''Ndege nao wanaupenda kwa sababu za usalama unaotoa kwenye viota vyao,”

Lakini Garba Sani, mtayarishaji filamu, anatoa onyo kuwa katika maeneo ya Kaskazini mwa Nigeria, ukubwa wa mti wa mbuyu unasababisha kutoweka kwake taratibu katika mitaa ya mijini.

“Kwa kuzingatia shina lake pana, mbuyu unachukuliwa kuwa mti unaopoteza nafasi katika mandhari ya ujenzi,” anasema.

Sani analalamikia jinsi watengenezaji wapya na wasanifu wa ardhi wanavyoharakisha kukata mibuyu mikubwa, na hivyo kusababisha kupungua kwa uwepo wake katika maeneo”.

Nyasha Chibanda, mtaalam wa maendeleo ya kimataifa mzaliwa wa Zimbabwe anayeishi Pretoria nchini Afrika Kusini, anatoa maoni tofauti.

“Katika jimbo la Masvingo, mashariki mwa Zimbabwe, mibuyu hukua zaidi katika maeneo ya mashambani yenye eneo kubwa la wazi. Wakaaji hawaoni sababu ya kuikata.”

Kando na kuwa ishara ya kitamaduni ya Afrika, uenezaji wa mbuyu barani Afrika unasalia kuwa kipaumbele kwa sababu bidhaa zake ni muhimu kwa makazi, chakula, lishe na uponyaji.

Tofauti na spishi zingine kubwa, miti hii ni sehemu ya maeneo ya makazi huku mizizi yake ikishuka chini badala ya kuchomoza kwa hiyo haiharibu misingi ya majengo.

Mti wa Mbuyu unaweza kukua urefu wa mita 30 angani Picha :AFP

Abdulkadir Musa, mwalimu mstaafu katika mji wa Giade wa Jimbo la Bauchi kaskazini-mashariki mwa Nigeria, anaonyesha jinsi umuhimu wa mbuyu katika ikolojia ya eneo hilo unavyovuka mwonekano wake wa kipekee.

Imani za jadi

"Majani ya mbuyu hutumika kama mboga au unga kama kiungo cha supu. Pia ni muhimu kama lishe. Mbegu zake huchomwa, na sehemu ya matunda huliwa mbichi au hutengenezwa maziwa, uji au juisi.

Gome la mti hutumiwa. kama nyuzi kwa ajili ya kufuma kamba, vikapu, na kuezeka paa," Musa anaiambia TRT Afrika.

Kuanzia mashamba hadi makazi, mbuyu husaidia dhidi ya mmomonyoko wa udongo, na wakulima hawaoni madhara yoyote katika mwavuli wa miti kuwa kivuli vamizi juu ya mashamba.

Local women process baobab fruit pulp into powder at a workshop that belongs to Baye fall community, in Ndem Picha : Reuters

Sani anataja kwamba katika ardhi ya Wahausa, majina ya baadhi ya maeneo yanatokana na mti wa mbuyu uliopo au uliokufa.

"Katika jiji la kale la Kano, mna maeneo kama Kuka Bulukiya na Kuka Uku. Kisha kuna Kukar Atillo katika mji wa Nahuce wa Toro, Jimbo la Jigawa," anasema.

Wakati mwingine , Mbuyu pia una sifa mbaya kitamaduni wakati mwingine ukihusushwa na ushirikina na mambo mabaya.

Baadhi ya dini za Kiafrika huhusisha viumbe au wafu kama vile kuabudu mababu, wageni, majini na mizimu. Katika baadhi ya jamii, mbuyu unachukuliwa kuwa "mti wa nje ya mji".

Ustahimilivu wa mabadiliko ya tabia nchi

Utamaduni wa Kihausa wa kabla ya Uislamu unaona mbuyu kama mkusanyiko wa majini, na watoto wanaonywa dhidi ya kupanda au kucheza karibu na mti kwa hatari ya kupandwa na mizimu. Ibada maarufu ya Bori ya uhuishaji wa Kihausa huangazia mbuyu katika desturi zake nyingi.

Madagaska ina aina nyingi zaidi ya mbuyu ulimwenguni. Picha: Reuters

Unaweza kuona mbuyu umekauka na kubakia gogo tu, lakini mara msimu ukibadilika, hubadili ghafla taswira yake na kuota majanimapya yenye kuvutia na kisha kuota matunda.

Ustahimilivu wa hali ya hewa wa mbuyu huruhusu kustawi. Hata inapokatwa kwa upande wake, inaendelea kuishi ikiwa imesalia na mizizi michache ardhini.

"Katika shina la mbuyu, hakuna utengano kati ya uti wake na sehemu ya pambapamba inayozingira kwa hivyo unaupa mtu uwezo wake wa kuhifadhi maji," anasema Dk Mustapha Karkarna, mratibu wa zamani wa Jimbo la Kano wa utafiti wa rasilimali za misitu wa Nigeria.

Kuna baadhi ya mibuyu ya kale ambayo yamechimbwa mashimo na wadudu na wanyama kama panya wanaofanya makao ndani yake.

Kulingana na Dk Karkarna, "shina zenye mashimo kwenye miti ya mbuyu husababishwa na magonjwa ya ukungu ambayo huharibu shina, sio kitu chochote kisicho kawaida".

Dk Karkarna anaamini sababu ya msingi katika kutoeleweka kwa mbuyu ni ukweli kwamba miti hii ni baadhi ya mimea ya zamani zaidi duniani

Mti mmoja wa mbuyu unaweza kuwa mzee kuliko mtu mzee zaidi katika jamii nzima. Hivyo, wanachukuliwa kuwa mashahidi wa siku za nyuma, na wana hadithi za kusimulia kuhusu historia ya jumuiya.

Mti wa mbuyu unaweza kuishi kuliko vizazi vya watu kwa sababu ya maisha marefu. Picha: AFP

Mti unapokua zaidi ya vizazi, unachukua ishara ya maisha marefu na hekima, na kuwafanya watu watoe tafsiri za kibinafsi kama vile kaburi la mizimu ya mababu. Mti huu hutumiwa katika hekaya na hekaya, ambapo wakati mwingine huangaziwa kama kaburi la uovu.

Tishio moja kubwa kwa kuwepo kwa mbuyu licha ya umuhimu wake katika ikolojia ya bara na tamaduni mbalimbali ni mandhari ya miji inayopanuka kwa kasi na upendeleo wa mimea ya kigeni kuliko spishi asilia za Kiafrika.

Lakini kama mwanafalsafa wa Ujerumani Friedrich Nietzsche alivyosema, kuishi ni kuteseka; kuishi ni kupata maana fulani katika mateso.

Hakuna jambo ambalo labda linatoa ushuhuda huu bora kuliko ushuhuda wa kale wa mbuyu wa milenia ya ukuaji wa ustaarabu na uharibifu.

TRT Afrika