Urusi yaongeza kampuni ya Meta kwenye orodha yake ya 'makundi ya Kigaidi'

Urusi imeongeza kampuni ya Meta ambayo inamiliki Facebook na Instagram kwenye orodha yake ya kampuni zinazounga mkono vitendo vya kigaidi.

Wamuzi huu sasa unaiweka Meta pamoja na makundi yote yanayodhaniwa kuwa ya Kigaidi nchini Urusi na yanayoeneza chuki dhidi ya Urusi katika mitandao ya kijamii.

Urusi inadiriki kusema kuwa vitendo vya chuki vinavyoelekezewa nchi hiyo vilianza pindi tu baada ya vita kuanza dhidi ya Ukraine.

Awali kampuni ya Meta tarehe 10 Machi ilisema itakubali jumbe kama “kifo kwa wavamizi kutoka Urusi” lakini baadae ikasema ni kwa ajili ya wanaotumia mitandao yake wakiwa ndani ya Ukraine.

Mitandao ya Facebook na Instagram haijakuwepo hewani nchini Urusi, jambo lililowalazimu watumiaji nchini humo kukimbilia VPN.

Instagram kwa mfano inapendwa sana nchini Urusi kwa ajili ya matangazo hasa ya kibiashara.

AFP