Kila anayejaribu kuingia akaunti ya Facebook ilirudi na jibu "Kipindi chako kimeisha," ikimwomba mtumiaji aingie tena upya kwenye akaunti.
Majaribio kadhaa ya kuingia tena hayajazaa matunda.
Kwenye Instagram, watumiaji walipokea ujumbe: "Haikuweza kuonyesha upya ukurasa" na "Haikuweza kupanadisha maudhui" walipojaribu kufikia akaunti zao.
Watumiaji wa Threads, mtandao mwingine wa kijamii unaomilikiwa na Meta, pia waliripoti matatizo.
Hashtag ya "Facebook Down" iliibuka kwenye mtandao wa kijamii wa X, zamani Twitter, Jumanne jioni.
Huduma ya ujumbe wa WhatsApp, ambayo pia inamilikiwa na Meta, hata hivyo, haikuripoti hitilafu ya aina yoyote.
Meta ilikuwa bado haijatoa mawasiliano rasmi kuhusiana na sababu ya usumbufu huo kufikia wakati wa stori hii kupanda hewani.