Mtandao wa Mozilla wenye makao yake makuu huko California ulikagua kampuni 25 za magari na kusema hakuna hata moja kati yao iliyokidhi viwango vyake vya faragha kikamilifu na kwamba hakuna aina nyingine ya bidhaa iliyopata matokeo duni ya ukaguzi.
"Magari ya kisasa ni jinamizi la faragha" wakati ambapo "watengenezaji magari wamekuwa wakijigamba kuhusu magari yao kuwa 'kompyuta kwenye magurudumu'", ilisema Mozilla, ambayo inajulikana zaidi kwa mtandao wake wa Firefox kinachojali usiri.
"Ingawa tuliyatilia wasiwasi kengele za milango yetu na saa zinazounganishwa kwenye mtandao kuwa ndio zinaweza kuwa zinatupeleleza, lakini magari yaliingia kimyakimya kwenye biashara ya data kwa kugeuza magari yao kuwa mashine zenye nguvu za kubana data," Mozilla ilisema.
Kulingana na utafiti, Tesla ilipatikana na dosari zaidi, nayo Nissan ilichukua nafasi ya pili na kuchaguliwa kwa kutafuta baadhi ya "aina za kutisha" za data, kama shughuli za ngono.
Utafiti huo uligundua kuwa asilimia 84 ya aina ya magari yalikiri kusambaza data ya kibinafsi ya watumiaji kwa watoa huduma, wakala wa data na biashara zingine ambazo hazijafichuliwa.
Wengi wao, asilimia 76, walisema waliuza data za wateja wao na zaidi ya asilimia 50 walisema kuwa walisambaza data na serikali na vyombo vya sheria pindi walipoambwa.
Idadi kubwa ya chapa za magari, asilimia 92, ziligunduliwa kutowapa wamiliki wake uwezo kamili wa kudhibiti data zao za kibinafsi na ni kampuni ya Renault ya Kifaransa pekee na chapa yake ya Dacia huruhusu watumiaji haki ya kufuta data, pengine kwa kufuata sheria za Umoja wa Ulaya.
Aidha, Mozilla ililalamika kuwa hakuna chapa yoyote ya magari ambayo pia ni pamoja na Ford, Chevrolet, Toyota, Volkswagen, na BMW ingethibitisha kuwa yanakidhi viwango vya chini vya usalama vya shirika hilo wakati asilimia 68 ilikabiliwa na uvujaji wa data, udukuzi au uvunjaji katika miaka mitatu iliyopita.