TikTok / Picha: Reuters Archive

Hiyo ni mojawapo ya hatua za hivi karibuni ya Muungano huo dhidi ya mienendo ya biashara ya magwiji wa teknolojia.

Faini hiyo, ambayo ni sawa na dola za kimarekani milioni 369, ni kufuatia kilele cha uchunguzi wa miaka miwili uliofanywa na Tume ya Ulinzi wa Takwimu ya Ireland (dpc).

Shirika la Ireland, lenye jukumu muhimu la kusimamia kanuni kali za usalama wa data za EU, liliipa TikTok miezi mitatu "kufanikisha utekelezaji wake" wa sheria.

Mnamo Septemba 2021, DPC ilianza kukagua uzingatiaji wa TikTok na GDP kuhusiana na mipangilio ya jukwaa na utekelezaji wa data binafsi kwa watumiaji walio na umri wa chini ya miaka 18.

Pia ilitathmini hatua za uthibitisho wa umri kwenye TikTok kwa watu wasiozidi umri wa miaka 13 bila kupata ukiukaji wowote. Hata hivo, iligundua jukwaa halikutathmini vizuri hatari kwa vijana wanaojisajili kwenye huduma hiyo.

Aidha, katika uamuzi wake wa siku ya Ijumaa, Mdhibiti pia aliangazia, jinsi watoto waliojiandikisha walivyokuwa na akaunti za TikTok zilizowekwa hadharani kwa chaguo-msingi, ikimaanisha kuwa yeyote angeweza kuangalia au kutoa maoni juu ya machapisho yao.

Samsung, TikTok

Pia iliikosoa huduma ya "kuunganisha familia" ya TikTok, ambayo imeundwa kuunganisha akaunti za wazazi na zile za watoto wao wa ujana, lakini DPC iligundua kampuni hiyo haikuthibitisha hali ya mzazi au mlezi.

Ireland iko katikati ya utawala wa GDPR kwa sababu Dublin ndio makao makuu ya Ulaya Ya TikTok na mashirika kama Google, Meta na X, zamani Twitter.

Mwezi Mei, DPC iliitoza Meta faini ya Euro bilioni 1.2 kwa kuhamisha data za watumiaji wa EU kwenda Marekani ikiwa ni ukiukaji wa uamuzi wa awali wa mahakama.

Tiktok, kitengo cha kampuni kubwa ya Teknolojia ya China ByteDance, ni maarufu sana miongoni mwa vijana ikiwa na watumiaji milioni 150 nchini Marekani na milioni 134 EU.

TikTok 'inatofautiana kwa heshima'

Ufikiaji unaowezekana wa utangazaji wa TikTok ungekuwa mkubwa zaidi katika Afrika Kaskazini kuliko Kusini mwa Afrika. Picha: Wengine

Ikizungumzia faini hiyo, TikTok ilisema "haikubaliani kwa heshima "na uamuzi huo, na ilikuwa" ikitathmini " jinsi ya kujitetea.

"Ukosoaji wa DPC unazingatia vipengele na mipangilio iliyokuwepo miaka mitatu iliyopita, na kwamba tulifanya ukarabati vyema kabla ya uchunguzi wake kuanza, kama vile kuziweka akaunti zote zisizozidi miaka 16 kwa faragha kwa chaguo-msingi," msemaji wa TikTok aliiambia AFP.

Jukwaa hilo linashikilia kuwa linafuatilia kwa karibu umri wa watumiaji wake na inachukua hatua inapohitajika.

TikTok inasema ilifuta takriban akaunti milioni 17 ulimwenguni ndani ya muda wa miezi mitatu ya kwanza ndani ya mwaka huu kwa sababu ya tuhuma za kumilikiwa na watu chini ya miaka 13.

Mapema mwezi huu, kampuni hiyo kubwa ya mtandao wa kijamii TikTok ilifungua kituo cha data kilichoahidi kwa muda mrefu huko Ireland, ikiwa na lengo la kujaribu kutuliza hofu huko Ulaya juu ya faragha ya data.

TikTok imekua katika mapato ya utangazaji na idadi ya watumiaji. Picha AP

Udhibiti kuu wa Ulinzi wa data GDPR, ulianza kutumika mnamo 2018 na ulikuwa na sheria kali na maarufu zaidi ya EU kuhusu teknolojia, ikihakikisha wananchi wanatoa idhini yao kwa njia ambazo data zao hutumiwa.

Faini ya ijumaa inakuja baada ya EU kuzindua orodha ya mabingwa wa dijitali wiki iliyopita pamoja na Apple, mmiliki wa Facebook meta na bytedance ambayo itakabiliwa na vizuizi vipya vya jinsi wanavyofanya biashara.

AFP