Mkurugenzi Mtendaji wa Tik Tok Shou Zi Chew alizungumza na kamishna wa Soko la ndani la EU, Thierry Breton, kupitia njia ya video. / Picha: AFP

TikTok imesema kuwa iliondoa video milioni nne "kwa ukiukaji" katika Jumuiya ya Ulaya mnamo Septemba, katika ripoti yake ya kwanza ya uwazi tangu sheria ya huduma za dijitali (DSA) ilipoanza kutumika katika Jumuiya hiyo.

"Tumeona mabadiliko kwenye jukwaa la TikTok katika miezi iliyopita, na vipengele vipya vinatolewa kwa lengo la kulinda watumiaji na uwekezaji uliofanywa kwa kiasi cha maudhui na uaminifu na usalama," Thierry Breton, kamishna wa soko la Ndani la EU, alisema, kupitia mawasiliano ya njia ya simu ya video na Mkurugenzi Mtendaji wa TikTok Shou Zi Chew.

Breton alisema Tume ya Ulaya ilikuwa ikichunguza iwapo TikTok imefanya vya kutosha kufuata sheria ya huduma za mitandao ya kijamii (DSA), baada ya kufungua uchunguzi mwezi uliopita.

"Sasa zaidi ya hapo awali, hatupaswi kuacha juhudi zozote za kuwalinda raia wetu haswa watoto na vijana dhidi ya yaliyomo na habari potofu," aliongeza.

Theo Bertram, makamu wa rais wa sera za umma wa Tiktok Uropa, alisema Breton na Chew walikuwa na "majadiliano mazuri juu ya maendeleo ya TikTok" kwenye sheria ya huduma za mitandao ya kijamii (DSA).

"Tunahimizwa kwamba juhudi zetu hazijatambuliwa. Tunaendelea kushirikiana kwa karibu na Tume ya kufuata huduma za mitandao ya kijamii DSA, " Bertram alisema kupitia mitandao ya kijamii.

"Ninafurahi kwamba juhudi za TikTok kufuata sheria ya huduma za mitandao ya kijamii (DSA) na kuweka jamii yetu salama, zinatambuliwa," Alisema Caroline Greer, Mkurugenzi wa Sera ya Umma wa TikTok.

Mkurugenzi Mtendaji wa TikTok, Chew anatarajiwa kukutana na makamishna wa EU, Vera Jourova na Didier Reynders mjini Brussels kujadili masuala mbalimbali pamoja na ulinzi wa data na vizuizi vipya vya Brussels juu ya nguvu ya soko la makampuni ya teknolojia.

AFP