Serikali ya Kongo na Zambia zimetia saini jana mkataba wa upembuzi yakinifu wa kutengeneza betri za magari zinazotumia lithiamu kwa njia yakujenga kiwanda katika sehemu ya kusini mashariki mwa Jamhuri yakidemokrasia ya Kongo.
Nchi hizo mbili za Afrika zitakuwa na betri ya magari na sekta ya nishati mbadala. Eneo la takriban hekta za mraba 2000 litajengwa katika Mkoa wa Katanga kwenye mpaka kati ya DRC na Zambia ili kushughulikia sekta hii.
Mkataba huu wa utengenezaji wa betri za magari ulikuwa umetiwa saini mbele ya waziri wa Viwanda wa DRC, Julien Paluku Kohongya, na mwenzake wa Zambia, Chipoka Mulenga, Waziri wa biashara na Viwanda Zambia.
Utafiti wa mradi huu unaweza kugharimu dola elfu 700 na unaweza kufadhiliwa na Benki ya African Import-Export (Afreximbank). Matokeo yanategemea kutoka mwezi wa nane.
TRT Afrika iliongea na Julien Paluku Kahongya, Waziri wa Viwanda wa DRC, ambaye alithibitisha kuwa mradi huu utajengwa katika eneo lisilo na kodi ili kuvutia wawekezaji ambao bado wanaogopa kuja kuwekeza nchini DRC kutokana na kodi nyingi.
"Tungependa kufanya ubunifu ili kuweza kuendana na teknolojia mpya ya kimataifa - Tunafanya utafiti na maendeleo ambayo yanatuonyesha kuwa baadhi ya malighafi ambazo tunazo chini ya ulinzi zina nguvu zaidi zikitumika kama betri," alisema Waziri Kahongya.
Ushirikiano huu unalenga kuendeleza mnyororo wa thamani wa kikanda kati ya nchi zinazo lenga soko la magari ya umeme na nishati safi ambayo inaweza kuleta faida ya mabilioni ya dola kwa nchi zote mbili.
Lithiamu hutumika katika utengenezaji wa betri za kisasa kwa teknolojia zinazoibuka na ni muhimu kama nishati safi.
Wiki iliyopita mashapo ya lithiamu pia yalipatikana Kaskazini mwa Tanzania na kampuni ya Marekani ya Titan Lithium Inc.
DRC inataka kuvutia faida kubwa zaidi kutoka kwa soko hili la kimataifa, linalowakilisha zaidi ya dola bilioni 800 ifikapo mwaka 2025. Licha ya operesheni kadhaa haramu za uchimbaji madini nchini DRC, serikali ya Jamuhuri wakidemokrasia ya Kongo inadai kuwa ni nchi yenye ushindani mkubwa zaidi wa kuzalisha betri za umeme.