"Zoezi la kuwarejesha watanzania walio nchini Sudan si jepesi" Waziri wa mambo ya nje Tanzania

"Zoezi la kuwarejesha watanzania walio nchini Sudan si jepesi" Waziri wa mambo ya nje Tanzania

Serikali ya Tanzania imeendelea na jitihada za kuwarejesha Watanzania kutoka Sudan kufuatia mapigano yanayoendelea nchini humo
Waziri wa mambo ya nje Tanzania

Serikali ya Tanzania kupitia waziri wake wa mambo ya nje Mhe. Dkt. Stergomena Tax imesema kuwa inaendelea na zoezi la kuwaondoa raia wake waliokwama Sudan lakini inathibitisha zoezi hilo si jepesi.

"Zoezi la kuwarejesha watanzania waliopo nchini Sudan si jepesi kwani viwanja vya ndege hususan Khartoum ambako ndiko kwenye mapigano vimefungwa". anasema waziri Stargomena Tax

Kufuatia siku tatu zilizotolewa za kusitisha mapigano (kati ya tarehe 21 23 Aprili Tanzania imeweka wazi kuwa tarari imefanikisha kuwaondoa raia wake katika eneo la vita Sudan.

"Tumeweza kuwasafirisha watanzania 200 (wanafunzi, watumishi wa Ubalozi, na raia wengine) kupitia mpaka wa Matema, Ethiopia kwa magari na wote wapo salama", alisema Dkt. Tax

Dkt. Tax ameongeza kuwa Watanzania hao watasafirishwa kwa ndege ya Shirika la ndege la ATCL kuja Tanzania.

"Ndege hiyo ipo tayari kuwachukuwa na kuwarejesha nyumbani".

Waziri huyo anasesitiza kuwa zoezi la kuwaondoa raia wa Tanzania limefanyika kwa ushirikiano na taasisi mbali mbali za ndani

Taasisi hizo ni pamoja na; Ofisi ya Rais, Balozi za Tanzania nchini Sudan, Ethiopia na Misri na pia Shirika la ndege la serikali ATCL.

TRT Afrika