Zaidi ya watu 40 wameuwawa ndani ya kipindi cha wiki moja katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kufuatia vurugu zilizoibuka kati ya pande zinazohasimiana katika magharibi mwa DRC.
Mauaji hayo yalihusisha vikundi vya Teke na Yaka, jeshi la nchi hiyo limesema.
Siku ya Ijumaa, jeshi la nchi hiyo lilivamiwa na kikundi cha wanamgambo wa Yaka katika jimbo la Kwango, na kusababisha vifo vya watu wapatao 21, wakiwemo wanajeshi wawili, kulingana na msemaji wa jeshi hilo Antony Mualushayi.
Mapigano hayo yalichochea vurugu kubwa zilizosababisha watu 12 kuchomwa moto.
Nyumba kuchomwa moto
"Waliwafungia watu ndani ya nyumba na kisha kuiwasha moto," alisema Guy Mosomo, mbunge wa eneo hilo.
TRT Afrika