Msumbiji imeshuhudia machafuko tangu uchaguzi mkuu wa Oktoba 2024, baada ya upinzani nchini humo kukataa matokeo rasmi ya uchaguzi mkuu ambayo yanakirudisha chama tawala cha FRELIMO madarakani/ Picha : Reuters

Ghasia za magereza katika mji mkuu wa Maputo wa Msumbiji zilisababisha vifo vya watu 33 na wengine 15 kujeruhiwa, amesema Kamanda Mkuu wa Polisi wa nchi hiyo Bernardino Rafael.

Haya yalijiri wakati wa machafuko ya ndani yanayohusishwa na matokeo ya uchaguzi wa Oktoba 2024 wenye utata yakiendelea.

Upinzani nchini humo umeyakataa matokeo rasmi ya Uchaguzi Mkuu ambao unakirudisha madarakani chama tawala cha FRELIMO.

Uamuzi wa Jumatatu (Disemba 23) wa mahakama ya juu ya Msumbiji kuthibitisha ushindi wa chama tawala kwa muda mrefu cha FRELIMO katika uchaguzi umeibua maandamano mapya nchini kote ya makundi ya upinzani na wafuasi wao ambao wanasema kura iliibiwa.

Takriban watu 1,534 walitoroka gerezani katika tukio hilo lakini 150 sasa wamekamatwa tena, Polisi wamesema, akiongeza kuwa kulikuwa na majaribio ya kuvunja magereza katika magereza mengine mawili.

Wanajeshi wasaka wafungwa

Msumbiji inasema oparesheni ya kuwatafuta inayoungwa mkono na jeshi, inaendelea kuwakamata wafungwa zaidi ya 1,500 waliotoroka jela ya Maputo siku ya Krismasi.

Mamlaka zilisema wafungwa waliotoroka walichukua fursa ya siku tatu za machafuko yaliyosababishwa na uthibitisho tata wa chama tawala cha Frelimo kama mshindi wa uchaguzi wa hivi majuzi Jumatatu.

Picha zilizonaswa kwenye mitandao ya kijamii zilionyesha makundi makubwa ya watu wakikusanyika na kukimbia katika eneo la gereza huko Maputo.

Kelele zilisikika na watu walionekana wakikimbia upande uleule mwishoni mwa video.

Reuters iliweza kuthibitisha eneo kutoka majengo ya karibu, nguzo za matumizi, rangi ya paa na kuta zinazolingana na picha za setilaiti.

Wakati Rafael akilaumu maandamano nje ya gereza hilo kwa kuchochea ghasia hizo, Waziri wa Sheria Helena Kida alikiambia kituo cha televisheni binafsi cha Miramar TV kwamba machafuko hayo yalianzishwa ndani ya gereza hilo na hayana uhusiano wowote na maandamano nje.

Takriban watu 1,534 walitoroka gerezani katika tukio hilo lakini 150 sasa wamekamatwa tena, Polisi imesema, akiongeza kuwa kulikuwa na majaribio ya kuvunja magereza katika magereza mengine mawili.

TRT Afrika