Ajali za barabarani kote nchini zimeangamiza maisha ya watu 649 tangu mwaka uanze.
Hii ni kulingana na takwimu kutoka kwa Mamlaka ya Kitaifa ya Usafiri na Usalama kati ya Januari 1 hadi Februari 20, 2024.
Takwimu hizi zimeongezeka ikilinganishwa na 623 zilizorekodiwa katika kipindi kama hicho mwaka wa 2023.
Wanaotembea kwa miguu wanaongoza kwa vifo kwa 252, ikilinganishwa na 190 iliyorekodiwa mwaka jana.
Waendesha pikipiki walirekodi vifo 152 na hii ni chini ya idadi ya177 mnamo 2023.
Mnamo 2024, angalau abiria 125 wamepoteza maisha katika ajali za barabarani ikilinganishwa na 114 mnamo 2023.
Baadhi ya madereva 43 wamepoteza maisha katika ajali za barabarani mwaka huu.
Hii ni chini ya idadi ya 59 katika kipindi kama hicho mwaka jana.
Abiria wa bodaboda 61 nao walipoteza maisha yao katika ajali ikilinganishwa na 71 vilivyoshuhudiwa mwaka jana.
Ajali za barabarani imekuwa changamoto pia kwa nchi jirani ya Tanzania ambapo serikali pia zinatoa tahadhari kwa wananchi kuwa waangalifu zaidi.