Picha zilizosambazwa  na vyombo vya habari vya serikali zilionyesha mamia ya watu karibu na eneo lenye uharibifu la udongo ulioporomoka. / Picha: AP

Zaidi ya watu 140 wamepoteza maisha kutokana na maporomoko ya udongo katika eneo la mbali kusini mwa Ethiopia siku ya Jumatatu, mamlaka za eneo zilisema, zikionya kwamba idadi ya vifo inaweza kuongezeka.

"Zaidi ya miili 140 imepatikana kutokana na maporomoko hayo," taarifa kutoka Idara ya Masuala ya Mawasiliano ya eneo la Gofa ilisema, ikimnukuu chifu wa eneo hilo Dagmawi Zerihun, ambaye alionya "idadi ya vifo bado inaweza kuongezeka."

Maporomoko ya ardhi yalitokea mwendo wa saa 10 asubuhi (0700 GMT) kufuatia mvua kubwa katika eneo la milima la jimbo la Ethiopia Kusini, Dagmawi alisema.

Wanawake na watoto walikuwa miongoni mwa waliopoteza maisha, alisema, akiongeza kuwa utafutaji wa manusura ulikuwa "unaendelea kwa nguvu."

Tukio la uharibifu mkubwa

Picha ambazo kwenye Facebook na chombo cha habari kinachoshirikiana na serikali cha Fana Broadcasting Corporate zilionyesha mamia ya watu karibu na eneo lenye uharibifu la udongo mwekundu ulioporomoka.

Picha hizo zilionyesha watu wakitumia mikono mitupu kuchimba uchafu katika kutafuta manusura.

Ukanda wa Gofa ni takriban kilomita 450 (maili 270) kutoka mji mkuu Addis Ababa, mwendo wa takriban saa 10, na unapatikana kaskazini mwa Mbuga ya Kitaifa ya Maze.

Jimbo la kanda ya Kusini mwa Ethiopia limeathiriwa na mvua fupi za msimu kati ya Aprili na mapema Mei ambazo zimesababisha mafuriko na watu wengi kuhama makazi yao, kulingana na shirika la Umoja wa Mataifa la kukabiliana na misaada ya kibinadamu OCHA.

Maporomoko ya ardhi ya kutisha

OCHA Ilisema mwezi Mei kwamba "mafuriko yaliathiri zaidi ya watu 19,000 katika maeneo kadhaa, na kuwafanya zaidi ya elfu moja kuyahama makazi yao na kusababisha uharibifu wa maisha na miundombinu."

Eneo la kusini limekumbwa na maporomoko ya ardhi hapo awali, na takriban watu 32 waliuawa mnamo 2018 baada ya maporomoko mawili tofauti ndani ya wiki moja.

TRT Afrika