Watu wanaoishi na ulemavu wa ngozi yaani 'albinism' nchini Uganda wanataka Tume ya Fursa Sawa (EOC) ibaki huru. Picha  @AfricaAlbinism 

Watu wanaoishi na ulemavu wa ngozi yaani 'albinism' nchini Uganda wamekataa pendekezo la Serikali la kuunganisha Tume ya Haki za Kibinadamu ya Uganda (UHRC) na Tume ya Fursa Sawa (EOC), wakisema kufanya hivyo kutaongeza zaidi unyanyapaa wanaokabiliana nao katika jamii.

Msimamo wa kundi hilo ulitolewa na Olive Namutebi, Mkurugenzi Mtendaji wa Muungano wa Mashirika yanayotetea wenye ulemavu wa ngozi.

Namutebi alikuwa mbele ya Kamati ya Sheria na Masuala ya Bunge kuwasilisha maoni ya kikundi kuhusu Muswada wa Marekebisho ya Katiba, 2024 inayotaka kuunganisha Tume hizo mbili kuwa chombo kimoja kiitwacho Tume ya Haki na Fursa Sawa.

"Gharama ya kuwatenga watu hawa waliotengwa kwa kupunguza mamlaka ya Tume ya Fursa sawa ni kubwa. Gharama ya kutengwa haiwezi kuchuma mapato yoyote. Inakupasa kujua kukosekana kwa usawa na chuki zinazopatikana kwa jamii zilizotengwa ambazo haziwezi kutatuliwa na mawakili au mahakama,” Namutebi alisema.

"Historia ya Uganda ina sifa ya migogoro ya kikabila, kidini na kisiasa ambayo imesababisha kutengwa na kubaguliwa kwa kundi moja dhidi ya jingine. Kwa hivyo, swali la ni je, ukatili, usawa wa kihistoria na uhalali uliosababisha kuundwa kwa Tume ya Fursa Sawa umefikiwa au la? Ukweli unaonyesha kuwa ukosefu wa usawa katika masuala ya kijinsia, kikanda, kisiasa, kijamii na kiuchumi bado upo," Namutebi alisema.

Jumuiya ya watu wenye ulemavu wa ngozi ililiomba Bunge kudumisha hali hiyo kwa hoja kwamba Tume ya Fursa Sawa imedhihirisha dhamira yake kwa jamii zilizotengwa.

Jumuiya hiyo imetoa mfano wa kisa ambapo shule binafsi ilibagua mwanafunzi mwenye wenye ulemavu wa ngozi na asasi ya kiraia ilifungua kesi na Mahakama ya EOC ilihakikisha haki ikitendeka. Walimu katika shule hiyo walipata mafunzo ili kujua kwamba wanafunzi watakuja wakiwa tofauti lakini maadamu wao ni binadamu na wamelipa karo ya shule, watendewe usawa.

"Nimekuwa na majadailiano na Tume ya Haki ya Uganda UHRC. Inaonekana kipaumbele chao ni ya masula ya kitaifa. Kwa hivyo, masuala ambayo yanaonekana kuwa madogo, kutengwa katika suala hili, kama mtoto mwenye 'ualbino' kutengwa shuleni, kwao idadi haijumuishi," Namutebi ameambia kamati ya bunge.

TRT Afrika