Shekhe Mustafa Rajabu, sheikh wa Mkoa wa Dodoma, Tanzania.

Na Ronald Sonyo

Sherehe hizo zitaanza Jumatano jioni katika viwanja vya Jamhuri baada ya swala ya Isha (Saa mbili usiku) kumalizika. Mbali na wageni kutoka ndani ya nchi ya Tanzania wengine ni kutoka nchi ya Kenya, Rwanda ,Burundi pamoja na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Sheikh wa Mkoa wa Dodoma Mustafa Zuberi, Maulid ameambia TRT Afrika kuwa maandalizi yamekamika kwa asilimia 100.

“Alhamdullih maandlizi yapo vizuri kuanzia itifaki, malazi, mapokezi na uwanja wa kufanya maulid pamoja na baraza la maulid limekamilika,” alisema Sheikh Zubeir.

Hata hivyo ameongeza kuwa wanawake na vijana pia watatumia fursa hii kuwatembelea wagonjwa waliopo katika hospitali ili kuwafariji na kuwaombea dua, kuambatana na mafundisho ya dini ya Kiislamu.

Mbali na wageni kutoka ndani ya nchi ya Tanzania wengine ni kutoka nchi ya Kenya, Rwanda ,Burundi pamoja na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo./ Picha TRT Afrika

Mufti Mkuu wa Tanzania Shekhe Abubakar Zuber Bin Ally ndiye mgeni maalum katika sherehe hizo huku Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akitarajiwa kulihutubia Baraza la Maulid.

Siku tatu zilizopita waumini wapatao 2000 walikusanyika katika kongamano maarufu la IJTIMAI, katika msikiti wa Gadafi kukumbushana mambo mbalimbali kuhusu imani ya dini ya kiislamu ikiwemo kutunzwa kwa maadili ya kitanzania na mafundisho ya ndoa.

TRT Afrika