Sudan Kusini inatarajiwa kuondoa wanajeshi 287 nchini DRC kufikia mwisho wa tarehe 8 / Photo: Reuters

Takriban wanajeshi 250 wa Sudan Kusini waliondoka Goma siku ya Ijumaa, kundi la hivi punde zaidi kutoka kwa jeshi la kanda ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kujiondoa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo baada ya Kinshasa kukataa kuongeza mamlaka yake.

Viongozi wa kijeshi wa serikali za nchi ya EAC walifanya mkutano mjini Ariusha tarehe 6 kujadili jinsi ya kuondoa majeshi yao DRC.

" Serikali zilizotuma wanajeshi DRC zinafaa kuaza kuondoa majeshi yao kutoka Mashariki wa DRC kufuatia mpango wa kuondoka uliowekwa," taarifa kutoka kwa Jumuiya ya EAC imesema.

Kenya tayari imeondoa maofisa 300  kutoka DRC / Picha:AFP 

" Kenya tayari imeondoa maofisa 300 huku Sudan Kusini inatarajiwa kuondoa wanajeshi 287 kufikia mwisho wa leo (tarehe 8)," taarifa hiyo imeongezea.

Jumuiya ya EAC ilipeleka wanajeshi wake katika eneo lililokumbwa na ghasia mnamo Novemba 2022, kwa mwaliko wa mamlaka ya DRC, kwenda kukomboa maeneo yaliyochukuliwa na kundi la waasi la M23.

Lakini mustakabali wa kutumwa kwa wanajeshi hao ulitiwa shaka baada ya Rais Felix Tshisekedi na wakaazi wa eneo hilo kushutumu jeshi hilo kwa kuishi pamoja na waasi badala ya kuwalazimisha kuweka silaha chini.

Wanajeshi wa Burundi wnatarajiwa kumaliza kuondoka nchini DRC kufikia tareje 7 Januari mwaka ujao. Picha Reuters 

" Wanajeshi wa kikosi cha jumuiya watakaobaki wakiwemo wa Uganda na Burundi wataendela kuondoka maifisa kupitia ndege na vifaa vyao kuitia barabara kati ya tarehe 8 Disemba na tarehe 7 Januari 2024," Jumuiya imeongeza katika taarifa.

Mataifa wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wameidhinisha kutumwa kikosi cha kulinda amani kama mchango wao katika kutafutia suluhu mzozo wa Jamahuri ya Demokrasia ya Congo, DRC.

TRT Afrika