Waananchi wengi DRC wanaogopa kurudi nyumbani Goma , DRC / Picha: Reuters

Francine Nsengiyumva ni mjane na pamoja na watoto wake watatu wana chakula kidogo huku wakilala kwenye udongo mgumu.

Lakini kama wengine wengi katika kituo cha kuhama kwa muda mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo anaogopa kurejea nyumbani.

"Wale waliochukua ardhi yetu bado wapo, bado wanaua watu na kufanya vitisho," alisema, akipika sufuria ya maharagwe kwenye moto.

Siku ya Jumapili, yeye na wanawake wengine na watoto walikusanyika nje katika kituo hicho, shule katika wilaya ya Lac Vert ya Goma, jiji lililotekwa na waasi wa M23 wiki iliyopita katika hali mbaya zaidi ya mapigano katika eneo hilo katika zaidi ya muongo mmoja.

Waasi hao wanataka kuonyesha wanaweza kurejesha utulivu na wamewataka raia kurejea katika maisha ya kawaida, lakini Nsengiyumva mwenye umri wa miaka 23 alisema haitakuwa salama kurejea katika kijiji chake cha Nzulo, karibu na Goma.

"Tutarudi tu wakati kuna amani."

Umoja wa Mataifa ulishutumu kikundi cha M23 na jeshi la DRC kwa ukiukaji mkubwa wa hivi majuzi wa haki za binadamu. Vikundi hivyo havijajibu swala hili. Utulivu unaripotiwa kurejea Goma baada ya kutekwa kwake. Lakini hakuna upande unaoonekana kuwa tayari kuweka silaha chini .

Wakati huo mapigano yameendelea katika eneo jirani ya Kivu Kusini, ambako waasi wanataka kuingia.

Changamoto ya magonjwa

Shirika la Chakula Duniani, WFP, linasema mgogoro wa kibinadamu huko Goma unazidisha wasiwasi juu ya mlipuko wa Mpox.

" Kufikia Januari 30, ni kesi 15 tu kati ya 143 zilizothibitishwa ambazo zilibaki kutengwa. Wengi wamekimbia vituo vya matibabu huko Goma na Nyiragongo, ambavyo vingine viliporwa.: WFP ilisema.

Imesema kuwa shughuli za kukabiliana na Mpox lazima zianze haraka.

" Chakula kinaisha. Maji ni haba. Hospitali zimezidiwa. WFP iko tayari kuanza tena usaidizi wa chakula punde tu ikiwa salama. Lakini tunahitaji ufikiaji wa kibinadamu sasa," WFP imeongezea.

Shirika la Umoja wa mataifa , UNOCHA DRC ndiyo iliyoathiriwa zaidi na kesi zaidi ya kipindupindu ikiwa watu 31,000 wameathiriwa.

TRT Afrika