Jitihada za kuweka makubaliano ya kumaliza uharibifu wa mazingira duniani kupitia plastiki zinaendelea jijini Nairobi, huku mataifa mengi duniani, pamoja na makampuni ya mafuta, wanamazingira na wengine walioathirika na uharibifu huo wanakusanyika kujadili makubaliano ya pamoja kwa mara ya kwanza.
Huu ni mkusanyiko wa tatu, katika vikao vitano vyenye lengo la kukamilisha majadiliano kufikia mwisho wa mwaka ujao.
Miendeno ya nguvu na nafasi yalikuwa wazi katika duru ya pili ya mazungumzo 'mini Paris na Punta del Este, Uruguay' na vimeonyesha nafasi inayofanana na ile ya mazungumzo ya kimataifa ya mabadiliko ya tabia nchi, na jambo jema ni kwamba, wahusika wote ni hao hao.
Plastiki ambazo zinatengezwa kutokana na mafuta ghafi na gesi asilimia, zinaipa nchi zinazozalisha mafuta nafasi kubwa katika makubaliano hayo.
Wahusika wakuu wa ulimwengu mara ya mwisho walikutana Paris mwezi June na kukubaliana kutengeza makubaliano ya kwanza kabla ya kukutana mjini Nairobi.
Rasimu ya kwanza ilipigwa chapa mwanzoni mwa September. Kamati ya Umoja wa Mataifa ya majadiliano ya kiserikali kuhusu uharibifu wa mazingira kupitia plastiki inajukumu la kutengeza makubaliano ya kwanza, ya kisheria kuhusu uharifu wa mazingira ardhini na baharini.
Marufuku ya Plastiki
Nairobi ni eneo muhimu la kufanya mkutano huu wa tatu, huku nchi hiyo ya Afrika Mashariki ikiongoza kwa kupambana na uharibifu wa mazingira wa plastiki, AP imeripoti.
Katika hatua muhimi mwaka 2017, Kenya ilipiga marufuku utengezaji, uuzaji na utumiaji wa mifuko ya plastiki, ambayo ilikuwa maarufu kwa kubebea bidhaa lakini pia ilikuwa imetapakaa kila sehemu ya mji.
Katika hatua kali zinazohusiana na marufuku hiyo, ni pamoja na wanaovunja sheria kukabiliwa na adhabu ya kifungo cha mpaka miaka 4.
Miaka miwili baadae, Kenya ilipiga marufuku matumizi ya plastiki katika vitu kama vijiko na mirija katika mabustani, misitu, fukwe na maeneo mengine yanayolindwa.
Kenya pia ni nchi muhimu katika masuala ya mazingira ikiwa ni makao makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Mazingira HABITAT.
Kenya inazalisha zaidi ya asilimia 70 ya nishati yake kutoka vyanzo mbadala.