Serikali ya DRC bado inapambana dhidi ya vuguvugu la kikundi cha waasi cha M23\AP

Mapigano yameongezeka katika siku za hivi karibuni karibu na mji huo, ambao uko takriban kilomita 20 (maili 12) kutoka Goma, mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kaskazini.

Wakazi wa Sake waliliambia AFP kwa njia ya simu kwamba vita hivyo vilikuwa vikiendelea kwenye vilima vinavyolitazama eneo hilo.

"Licha ya hali hiyo, tunadhibiti mji wa Sake," chanzo cha usalama kilisema, baada ya mapigano makali ya jumatatu.

"Mapambano bado yanaendelea muda huu," chanzo hicho kiliongeza.

Kulingana na Meya wa eneo hilo, Maombi Mubiri idadi kubwa ya wakazi wamekimbia kwa ajili ya usalama wao.

"Kwa sasa, waasi wanashikilia sehemu ya kusini ya eneo hilo la Sake, wakati kikundi cha Wazalendo, kiko upande wa Kaskazini," Meya huyo alisema.

Mtoa huduma ya Afya wa eneo hilo alisema kuwa milio mingi ya risasi ilisikika eneo hilo, huku watu watatu wakijeruhiwa, kutibiwa na kuhamishiwa kwenye mji wa Goma.

"Mji bado haujatwaliwa na waasi," kilisema chanzo hicho ambacho kiliomba jina lake lihifadhiwe.

AFP