Mzozo ambao umedumu kwa miongo kadhaa umesababisha mamilioni ya watu kuyahama makazi yao mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. / Picha: Reuters

Takriban watu milioni moja katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamekimbia makazi yao mwaka huu, mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa alisema Jumanne.

Volker Turk alisema hali nchini humo inazidi kuwa mbaya siku baada ya siku, na alieleza hofu yake kutokana na kuongezeka kwa idadi ya wanaosubiri kunyongwa baada ya DRC kurudisha tena hukumu ya kifo iliyositishwa mwaka 2003.

Turk, ambaye alitembelea DRC mwezi wa Aprili, aliliambia Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa kwamba nchi hiyo ya Afrika ya kati inakabiliwa na "mchanganyiko wa kuongezeka kwa ghasia, maslahi ya kikanda na kimataifa, mashirika ya unyonyaji na utawala dhaifu wa sheria".

Alisema idadi ya wahasiriwa wa ukiukaji wa haki za binadamu inaendelea kuongezeka, huku asilimia 85 ya ukiukwaji uliofanywa katika eneo la mashariki lililoathiriwa na migogoro katika kipindi cha miezi 12 hadi Juni 1.

Makundi yenye silaha yanafikiriwa kuhusika na asilimia 61 ya ukiukaji huo. Baadhi ya waathiriwa wapya 700 wa unyanyasaji wa kingono walirekodiwa katika kipindi hicho.

Ukosefu wa chakula "Kulingana na vyanzo vya mashirika ya kibinadamu, watu 940,000 zaidi wamekimbia makazi yao mwaka huu, na kufanya jumla ya wakimbizi wa ndani kuwa zaidi ya milioni 6.4," Turk alisema.

Aliongeza kuwa watu milioni 23.4 walikuwa na uhaba wa chakula, ikimaanisha wanakosa upatikanaji wa mara kwa mara wa chakula salama na chenye lishe.

Turk alisema bado ana wasiwasi na kwa kurudishwa tena hukumu ya kifo mwezi Machi iliyositishwa tangu 2003, na kuiita "hatua kubwa nyuma".

Tangu wakati huo, wanaume 128 wamehukumiwa kifo na mahakama za kijeshi, alisema.

"Ninaomba mamlaka kuhakikisha kuwa hukumu hizi hazitekelezwi," Turk alisema.

MaliasiliKamishna mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa amesema DRC imebarikiwa kuwa na maliasili za kipekee, ikiwemo madini na msitu wa pili kwa ukubwa duniani.Hata hivyo, alisema "unyonyaji haramu na biashara haramu ya maliasili ya DRC, pamoja na ushirikiano wa makampuni...na usafirishaji wa silaha", ndiyo inayochochea ghasia za sasa."Hali hii pia inasukuma idadi ya watu katika umaskini. DRC ni mojawapo ya mataifa matano maskini zaidi duniani... hali hii haikubaliki," alisema Turk.Alisema unyonyaji huu ni sehemu ya maisha ya kila siku ya watu duniani kote, huku simu za mkononi zikiwa na madini kutoka mashariki mwa DRC.Katika uchaguzi uliofanyika Jumatano kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York, DRC ni miongoni mwa wagombea watano wa viti vitano vya Afrika katika Baraza la Haki za Kibinadamu kwa muhula wa miaka mitatu kuanzia mwaka ujao.

TRT Afrika