Bara Afrika lina idadi kubwa zaidi ya vijana duniani, huku zaidi ya 70% ya watu wake wakiwa chini ya umri wa miaka 30. Picha TRT Afrika Picha : TRT Afrika

Zaidi ya viongozi tisa wa Afrika wanatarajiwa kuhutubia kongamano la mtaji wa watu katika ukuaji wa uchumi wa kitaifa, jijini Dar es Salaam.

Kongamano hilo liliandaliwa na serikali ya Tanzania kwa ushirikiano na Benki ya Dunia kama mpango wa kuendeleza mazungumzo juu ya mambo muhimu ya serikali katika hitaji la kuvutia umakini wa jukumu la mtaji wa watu katika ukuaji wa uchumi na kuinua mjadala juu ya umuhimu wa kuwekeza kwa watu.

Miongoni mwa masuala yanayo ibua mjadala zaidi barani Afrika ni ukuzaji wa vipaji vya vijana vinavyoweza kuinua uwekezaji na uzalishaji ndani ya nchi za Kiafrika.

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu UNFPA, Bara Afrika lina idadi kubwa zaidi ya vijana duniani, huku zaidi ya 70% ya watu wake wakiwa chini ya umri wa miaka 30. Idadi hiyo kubwa ya vijana ni fursa kwa ukuaji wa bara - lakini iwapo tu vizazi hivi vipya vitawezeshwa kikamilifu kutambua uwezo wao kamili.

Kenya Ramadan

Takwimu za Benki ya Dunia zinasema kuwa kufikia 2030, bara hili litakuwa na zaidi ya vijana milioni 600 chini ya miaka 25.

''Hii ni idadi kubwa sana ya wachapa kazi duniani. Ni muhimu kuwaandaa vijana hawa kwa umahiri kuweza kushindana katika ngazi ya kimataifa,'' anasema Benjamin Fernandes, mjasiriamali wa teknolojia nchini Tanzania.

''Mimi nipo katika sekta ya teknolojia na uhandisi wa programu, na nadhani tunatakiwa kuwainua vijana zaidi katika nafasi hizi ili waweze kutumika sio Tanzania pekee, bali kimataifa.'' Anaongeza Benjamin.

Mkutano huo utahimiza majadiliano ya kiufundi, kushiriki maarifa ya hivi punde kuhusu mtaji wa watu, na kuhitimisha kwa ahadi madhubuti na hatua zinazofuata kutoka kwa wakuu wa nchi wanaoshiriki.

''Kuna miradi mingi mfano nchini Rwanda na bila shaka nchi zingine za Afrika Mashariki pia, ambazo zinalenga kuinua biashara za wajasiriamali vijana, wake kwa waume,'' anasema Sharon Akanyana, mfanyabiashara wa Rwanda.

''Lakini biashara hizi zinatarajiwa kukua na kurudisha uwekezaji zaidi ndani ya nchi na kuleta pato. Kwa hiyo ni bora kama ni njia ya mikopo iwe mikopo iliyo nyepesi kwetu. Pengine watoze riba ya chini au hata watuondolee riba.'' anaongeza Sharon.

Mada kuu ya mkutano huu wa Dar ni 'Kuunganisha uwekezaji katika rasilimali watu na ukuaji wa uchumi' Picha TRT Afrika 

Lakini Aslata Nguku, dada kutoka Kenya anayeendesha mradi wa kuwasaidia wafanyabiashara wadogo, anahizmiza vijana kuwa namaono ya kujikuza zaidi.

''Kina mama wamekuwa wakifanya biashara kwa muda mrefu sana,'' anasema Aslata. ''Ila tu hatujapata mafunzo kuhakikisha biashara hazisalii kuwa ndogo, lazim atuhakikishe kuna namna zinaendelea kukua na kupanuka.'' ameongezea.

Mada kuu ya mkutano huu wa Dar ni 'Kuunganisha uwekezaji katika rasilimali watu na ukuaji wa uchumi'.

Na wakati viongozi wanatarajiwa kutangaza sera na maono yao juu ya kujumuisha rasilimali watu katika kuimarisha uchumi wa kitaifa, vijana nao wanasubiri kwa hamu kusikia nafasi yao itakuwa ipi kwani ndio kiasi kikubwa cha rasilimali watu.

TRT Afrika