Takriban vifaru 23,300 walizurura barani Afrika mwishoni mwa mwaka jana 2022 / Picha: AP

Takriban vifaru 23,300 walizunguka barani Afrika mwishoni mwa mwaka jana 2022, ikiwa ni ongezeko kwa 5.2% ya idadi iliyorekodiwa 2021.

Hii ni kulingana na Muungano wa Kimataifa wa Uhifadhi wa Mazingira (IUCN).

"Kwa habari hizi njema, tunaweza kupata ahueni kwa mara ya kwanza katika muongo mmoja," Michael Knight, mwanaikolojia wa wanyamapori ambaye ni mwenyekiti wa Kundi la Wataalamu wa vifaru wa kiafrika la IUCN, alisema.

Vifaru wameangamizwa kwa uhalifu unaoendeshwa na mahitaji makubwa kutoka Asia/ Picha : Others 

IUCN ilijumuisha makadirio ya vifaru kutoka mataifa mbalimbali ili hesabu za bara na kusema, "Mchanganyiko wa mipango ya uhifadhi na sababu za kibayolojia zimesababisha vifaru weusi kuongezeka kwa 4.2 asilimia na kufikia idadi ya vifaru 6,487.

Ana kwa vifaru weupe walikuwa juu kwa asilimia 5.6 hadi 16,803 kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2012," IUCN ilisema.

Zaidi ya vifaru 500 wauawa 2022

Hata hivyo, licha ya ongezeko hili, kumekuwa na changamoto ya vifaru kuuawa kutokana na vitendo vya majanjili wanaowawinda wanyama hao. Kuna mahitaji makubwa ya pembe za vifaru katika nchi za Asia, ambapo pembe zinatumiwa kutengeza dawa za jadi.

Zaidi ya vifaru 550 waliuawa na wawindaji haramu katika bara zima mwaka 2022, wengi wao wakiwa nchini Afrika Kusini, kulingana na IUCN.

Afrika Kusini ina takriban asili mia 80 ya vifaru duniani.

Wawindaji haramu huko wamezidi kulenga hifadhi zinazomilikiwa na watu binafsi katika msako wao wa pembe, zinazotafutwa sana katika masoko ya watu weusi ambapo bei kwa kila uzani inashindana na ile ya dhahabu na kokeini kwa wastani wa dola 60,000 kwa kilo.

TRT Afrika