Zaidi ya tembo 200,000 wanakadiriwa kuishi katika eneo la hifadhi lililoenea katika nchi tano za kusini mwa Afrika -/ Picha : Reuters

Namibia inapanga kuwaua wanyama pori 723, wakiwemo tembo 83, na kusambaza nyama za wanyama hao kwa watu wanaokabiliwa na na baa la njaa kutokana na ukame mkubwa kusini mwa Afrika, Wizara ya Mazingira ya nchi hiyo imesema.

Uwindaji huo utafanyika katika hifadhi na maeneo ya jamii ambapo mamlaka inaamini kuwa idadi ya wanyama inazidi eneo la malisho na maji, ilisema katika taarifa iliyotolewa Jumatatu.

Eneo la kusini la mwa Afrika linakabiliwa na ukame mbaya zaidi kuwahi kutokea kwa miongo kadhaa, huku Namibia ikiwa imemaliza asilimia 84 ya akiba yake ya chakula mwezi uliopita, kulingana na Umoja wa Mataifa. Karibu nusu ya wakazi wa Namibia wanatarajiwa kukumbwa na viwango vya juu vya uhaba wa chakula katika miezi ijayo.

Kutokana na ukame huo mkubwa, migogoro ya binadamu na wanyamapori inatarajiwa kuongezeka ikiwa mamlaka haitoingilia kati, Wizara ya Mazingira ilisema.

"Kutokana na hali hii, tembo 83 kutoka maeneo yenye migogoro chinjwa , (na) nyama itagawiwa kwa ajili ya mpango wa kukabiliana na ukame," wizara hiyo ilisema.

Nchi hiyo pia inapanga kuwaua viboko 30 na nyati 60, pamoja na swala pala 50, nyumbu 100 wa bluu, pundamilia 300 na wengineo.

Wanyama mia moja na hamsini na saba tayari wamewindwa na watalaamu wa uwindaji makampuni yaliyopewa kandarasi na serikali, na kutoa zaidi ya kilo 56,800 za nyama.

"Zoezi hili ni la lazima na linaendana na mamlaka yetu ya kikatiba ambapo maliasili zetu zinatumika kwa manufaa ya raia wa Namibia," wizara ya mazingira ilisema.

Zaidi ya tembo 200,000 wanakadiriwa kuishi katika maeneo ya hifadhi ndani ya nchi tano kusini mwa bara la Afrika, zikiwemo Zimbabwe, Zambia, Botswana, Angola na Namibia - na kufanya eneo hilo kuwa moja ya maeneo yenye Tembo wengi duniani kote.

Reuters