Uhusiano wa Uturuki na Afrika

Uturuki imeweka wazi mtazamo wake kwa nchi za kiafrika kuwa unaendana kikamilifu na kanuni za msingi za Umoja wa Afrika

Katika taarifa siku ya Alhamisi, Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki ilituma salamu za pongezi kwa waafrika wote.

"Tunawapongeza dada na kaka zetu wote wa Kiafrika kwa kuadhimisha siku ya Afrika ya Mei 25 ambayo inaadhimisha kumbukumbu ya miaka 60 ya kuanzishwa kwa Umoja wa Afrika ambayo unaowakilisha maadili ya watu wa Afrika kwa bara jumuishi, lenye amani na ustawi" ilifafanua taarifa hiyo

Mwaka huu, katika muktadha wa siku ya Afrika, maonyesho ya kazi za mikono ya kiafrika yatazinduliwa kwa ushirikiano na soko la sanaa za mikono la Afrika na jumba la utamaduni .

Majadiliano yenye mada ya "Mahusiano ya Uturuki na Afrika katika miaka mia moja ya jamhuri" yataandaliwa na ofisi ya rais kwa Waturuki nje ya nchi na jumuiya husika.

Kwa mujibu wa taarifa ya wizara, Balozi Burak Akçapar, naibu Waziri wa mambo ya nje, atatoa hotuba katika hafla ya kusherehekea itakayoandaliwa na mabalozi wa nchi za Kiafrika wanaoishi mjini Ankara ambapo mataifa 38 ya Afrika yanawakilishwa.

Katika kuadhimisha miaka 60 ya kuanzishwa kwa moyo wa kiafrika, Afrika imekuwa mhusika mashuhuri, shupavu na mhusika mkuu ndani ya jumuiya ya kimataifa.

"Kwa uelewa huu, tunaunga mkono kikamilifu juhudi za marafiki zetu wa Kiafrika kuelekea amani, utulivu na maendeleo pamoja na mipango inayolenga kuongeza uwepo wa Waafrika kwenye kongamano la kimataifa", taarifa hiyo ilifafanua

Ikitolea mfano mtazamo wa Ankara kwa nchi za Afrika, wizara hiyo ilisisitiza kuwa "mtazamo wetu kwa nchi za Kiafrika unaendana kikamilifu na kanuni za msingi za Umoja wa Afrika na unategemea ushirikiano kamili, jumuishi na sawa kwa misingi ya kuheshimiana na mkakati wa kushinda".

"katika matazamio ya 1963 na maono ya Afrika, na kuweka umuhimu mkubwa kwa ajenda 2063 na malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa 2030", iliongeza

Ankara iliahidi zaidi kuendelea kuimarisha ushirikiano na mshikamano wake na Afrika katika nyanja zote ambazo zimepanda hadi ngazi mpya kabisa kufuatia mkutano wa ushirikiano wa Uturuki-Afrika uliofanyika Uturuki tarehe 16-18 Desemba 2021 ndani ya upeo wa sera ya ushirikiano wa Afrika.