Nyati wa Kiafrika / Photo: Getty Images

Kenya imeidhinisha ulaji wa nyama ya nyati wa maji wanaofugwa .

Nyati hawa wamepewa jina hili kwa sababu wanapenda kukaa katika maeneo ya maji, na wanatumia muda mwingi wakiwa ndani ya maji, wakati mwingine maji yanafika hadi urefu wa pua.

Wanaweza kuwa na uzito wa hadi kilo 900 na fahali waliokomaa wanaweza kuwa na urefu wa kati ya mita 1.7 na 3.4.

Kuna aina moja tu ya nyati barani Afrika lakini aina nne tofauti zipo: nyati wa msitu, nyati wa savanna wa Afrika Magharibi, nyati wa Afrika ya Kati, na nyati wa savanna wa kusini.

Nyati wa kike hupata ndama wao wa kwanza wakiwa na umri wa miaka minne au mitano.

Kwa kawaida huzaa kila baada ya miaka miwili, na watoto wengi hutokea mwishoni mwa msimu wa mvua wakati nyasi nyingi huimarisha kiwango cha lishe kwa wanawake wanapokuwa wajawazito au wanaonyonyesha.

Wanaweza kuishi katika makundi wakiwa mamia lakini wamejulikana kukusanyika kwa maelfu katika mbuga ya Serengeti wakati wa mvua.

Kukusanyika katika makundi makubwa ni mojawapo ya kujikinga dhidi ya wanyama wanaowawinda kama simba.

Majike na watoto wao huwa wengi kwa makundi huku nyati wa kiume wakitumia muda mwingi wakiwa wenyewe.

Nyati wa maji hula nyasi za majini na mimea ya ardhi oevu inayofanana na nyasi.

Lakini msimu wa ukavu wanakula nyasi ya kawaida.Baada ya kula nyasi, kama vile ng'ombe, wao hutumia wakati wa kutafuna ili kutoa virutubisho zaidi kutoka kwa chakula chao.

Kwa ujumla nyati wana changamoto ya kuona na kusikia, lakini nyati wa kiafrika wana uwezo mkubwa wa kunusa.

Pia wanaonekana kuwa na wakati mgumu kiasi wa kudhibiti halijoto ya mwili—sababu kwa nini wanakula mara nyingi usiku.

Nyati hawa wa kiafrika wana uwezo wa kuishi kwa zaidi ya miaka ishirini, na kimsingi nyati barani anafahamika kuwa ishara ya nguvu, ustahmilivu na mwenendo wa kuwa kama jamii Kenya sasa itajiunga na nchi zingine zinazoruhusu nyama ya nyati kuliwa ambayo inasifika kwa kuwa na protini nyingi, kalori na mafuta ikilinganishwa na nyama ya ng'ombe.

TRT Afrika