Watu wanaounga mkono Palestina wamekuwa wakifanya kampeni ya kutaka vita visitishwe / Picha: AFP

Migogoro ya kivita, iwe baina ya nchi ama ndani ya nchi kwa kawaida huhusisha pande mbili au zaidi ambazo zinaweza kuwa na silaha.

Jitihada huwekwa mara kwa mara na washikadau tofauti kwa aajili ya kusimamisha vita ili kuepusha madhara ya maisha na mali.

Kuna aina tofauti ya usitishaji wa mapigano.

Usitishaji mapigano wa kibinadamu

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) inafafanua kusitisha kwa kibinadamu kama "kusitishwa kwa muda kwa uadui kwa madhumuni ya kibinadamu tu."

Nchini Sudan usitishaji wa mapigano miezi sita iliyopita kwa ajili ya kibinadamu kuliwawezesha watu kununua bidhaa sokoni / picha AFP 

OCHA pia inabainisha: “Kuhitaji makubaliano ya pande zote husika, kawaida ni kwa kipindi maalum na maalum eneo la kijiografia ambapo shughuli za kibinadamu zinapaswa kufanywa."

Kwa mfano Hamas na Israel yamefikia makubaliano na Hamas ya kubadilishana wafungwa. Jamii ya kimataifa imeendelea kuhimiza usistishaji wa mapigano kwa sababu za kibinadamu kwa ajili ya kuwezesha watu katika maeneo ya Palestina kupata misaada ya dharura.

Usitishaji mapigano wa upande mmoja

Kama jina linavyopendekeza, kusitisha mapigano kwa upande mmoja hutangazwa na chama kimoja cha mgogoro badala ya kwa mfano mazungumzo kati ya pande mbili zinazozozana.

Nchini Ethiopia wakati wa vita kati ya jeshi na kikundi cha Tigray People Liberation Front kati ya 2020 na 2022, usitishaji wa vita mara kwa mara ulisaidia mashirika ya misaada kufikia walioathiriwa / {Picha: AFP

Usitishaji huo wa mapigano unaweza kuwa bila vipengele vingi, au kwa muda maalum, kwa masharti ya upande mmoja.

Upande pinzani pia unaweza kutangaza kuridhiana na pendekezo la upande huo mwingine au kuamua kusitisha mapigano kwa masharti yao wenyewe na ahadi yao wenyewe.

Usitishaji mapigano kwa muda

Usitishaji mapigano wa muda umeanzishwa kwa muda mdogo, ambapo wahusika wote wa kambia zote kwa pamoja wanakubaliana na ahadi maalum, mara nyingi hutokea katika eneo maalum la kijiografia.

Makubaliano kama haya yanaweza kuongeza uaminifu miongoni mwa wahusika kama wao kujadili usitishaji mapigano kwa mapana zaidi.

Usitishaji mapigano baina ya nchi mbili

Usitishaji wa mapigano baina ya nchi mbili, au kati ya vyama viwili inaweza kuwa ya awali au ya uhakika na inaweza kushiriki sifa na usitishaji mapigano ya aina zingine.

Kwa mfano, jamii ya kimataifa inaendelea kuhimiza kuwe na usitishaji wa vita baina ya Ukraine na Urusi huku vita hivyo vikiendelea tangu Februari 24.

Usitishaji wa vita wa pande nyingi

Makubaliano ya kusitisha mapigano ya pande nyingi yanakubaliwa na pande tatu au zaidi za migogoro na inaweza kuwa ya awali au ya uhakika.

Mazingatio kwa usitishaji vita endelevu wa wadau mbalimbali ni pamoja na kuweka mipaka ya kijiografia katika maeneo, mipangilio ya maeneo yanayopishana ya udhibiti au ushawishi, na kupitishwa kwa mipangilio ya uhusiano, mawasiliano na uratibu.

Kwa mfano mwaka 2000, vyama 19 katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Burundi , vikiwemo vyama 17 vya siasa na vuguvugu la silaha, Serikali ya Burundi na Bunge - walitia saini Mkataba wa Amani wa Arusha na Mkataba wa Maridhiano na mbalimbali itifaki na viambatisho nchini Tanzania.

Wataalamu wanasema vyovyote vile, usitishwaji wa mapigano unaosimamisha ghasia kwa masaa, masiku au hata miezi utakuwa mwanzo tu wa kazi ngumu zaidi inayotakiwa kufanywa ili kuleta usalama wa maana na wa muda mrefu na utulivu kwa Wapalestina na Waisraeli.

TRT Afrika