Samia suluhu alizaliwa 27 Januari 1960. /Picha : Ikulu Tanzania 

Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametumia siku yake ya kuzaliwa kama ukumbusho kwa taifa wa uhifadhi wa mazingira.

''Upandaji wa miti kwa wingi pamoja na mikoko kutasaidia kurudhisha hali asilia ya bahari na kupunguza kasi ya mmomonyoko wa ardhi,'' amesema Mama Samia katik ataarifa iliyochapishwa katika mtandao wa ikulu wa X, zamani twitter.

Rais Samia aliungana na wananchi na makundi mbalimbali kupanda miti 4720, ikiwemo miti 120 ya matunda.

Miti hiyo imepandwa katika eneo la Donge Muwanda, jimbo la Tumbatu,

Mama Samia alilalamikia kasi ya uharibifu nchini humo hasa kisiwani Zanzibar.

Katika kutafutia suluhu, Mama Samia ameitaka ofisi ya makamu wa kwanza wa Zanzibar kuzuia uchimbaji wa mchanga kiholela pamoja na kusitisha shughuli za kukata matofali ya miamba na kutoa vibali vya uchimbaji kwa wananchi wanaokaa maeneo ya juu pekee.

TRT Afrika