Ngoma ya asili ya Rwanda Intore imetambuliwa na UNESCO kama urithi wa kimataifa / Picha kutoka UNESCO

Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limetambua ngoma ya asili ya Rwanda Intore, kama urithi wa kimataifa.

Intore huchezwa katika kundi.

Wachezaje wanapangwa katika mistari inayowakilisha safu za wapiganaji kwenye uwanja wa vita.

Kupitia mienendo yao, wao huiga vita na adui asiyeonekana, wakirukaruka na kushika mikuki na ngao zao kwa mdundo wa ngoma na pembe za kitamaduni.

Kupitia mienendo yao, wao huiga vita na adui asiyeonekana / Picha kutoka UNESCO

Mchezo wa ngoma ya Intore unaambatanishwa na mkono na nyimbo na mashairi ya ushindi na nguvu.

Wacheza ngoma ya Intore huchaguliwa kitamaduni na viongozi wao kupata mafunzo katika taasisi inayojulikana kama Itorero, ambapo walijifunza maadili ya kitamaduni, kanuni za utawala, ujuzi wa kuzungumza mbele ya watu, michezo ya kitamaduni na sanaa nyingine za maonyesho.

Siku hizi mazoezi hayo yameenea.

Kando na kuwa mcheozo wa kitaifa, ambao ni mazoezi katika kiwango cha kitaifa, vikundi vyengine vya wachezaji vimetawanywa nchini kote.

Vipindi vya mafunzo hupangwa mara kwa mara na shule na vyuo vikuu.

Utamaduni huu pia hupitishwa ndani ya familia na jamii.

Onyesho la ushindi na nguvu ya mchezo wa ngoma ya Intore iko katikati ya hafla na sherehe za jamii, ikijumuisha harusi, mapokezi ya wageni mashuhuri na sherehe ya mavuno.

Kuanzishwa kwa mashirika ya ngoma na uratibu wa tamasha na matukio ya kitamaduni ya ngoma hii imekuwa muhimu katika kukuza mshikamano wa kijamii wa Wanyarwanda.

TRT Afrika