Stévy Daic Ndjalala Totolo ni mtaalamu katika kutengeneza na kuumba sauti./Picha:  Stévy  

Na

Firmain Eric Mbadinga

Stévy Daic Ndjalala Totolo anatumia sauti yake kama mtaji wakati wa kutengeza vikaragosi, filamu kwa kutumia lugha za Kiafrika na za kimataifa.

Mwaka 2021, Stévy aliasisi kampuni ya Gemini Multimedia ya nchini Rwanda katika kudhirisha kipaji chake.

Stévy, ambaye ni mjasiriamali na mtaalamu wa mawasiliano, amejitengenezea mradi wa kibiashara ambao unazidi kujipatia umaarufu barani Afrika.

"Natokea Gabon na timu yangu imejaa watu wenye vipaji mbalimbali barani Afrika. Iwapo ikitokea kazi itakayohitaji maudhui ya lugha za Kihausa, Kiswahili, Kiyoruba au Kishona, basi huwa najaribu kuwapa wengine wenye uelewa mkubwa wa lugha hizo," anasema Stévy.

"Nafanya kazi na wazalishaji wa Kifaransa na sauti yangu pia hutumika katika maudhui ya lugha ya Kiingereza."

Stévy, ambaye ni mjasiriamali na mtaalamu wa mawasiliano, amejitengenezea mradi wa kibiashara ambao unazidi kujipatia umaarufu barani Afrika./Picha: Stévy 

Shughuli za kurekodi hufanyika katika studio yake iliyoko katika wilaya ya Kagugu, jijini Kigali.

Kwa sasa, studio ya Gemini ndio gumzo la mji pale Kigali, kutokana na ubora wa miundombinu yake.

"Makampuni mengi ya nje huachagua kufanya kazi na sisi kwani tunao uweza a ujuzi unaokubalika kimataifa," Stévy anaeleza.

"Gharama zetu ni nafuu zenye kufaidisha pande zote mbili."

Kati ya wateja wanaotumia huduma za Gemini ni pamoja taasisi za matangazo na mashirika yasiyo ya serikali.

Kwa sasa, studio ya Gemini ndio gumzo la mji pale Kigali, kutokana na ubora wa miundombinu yake./Picha: Stévy

Kusikia ni kuamini

Mara zote, wale wanaoingiza sauti kwenye vikaragosi na matangazo mengine hawahitaji kusoma, bali wanatakiwa tu kuvaa uhalisia wa wahusika hao.

Kulingana na mjasiriamali huyo, tasnia ya utengenezaji sauti inazidi kuwa maarufu barani Afrika.

Mmiliki huyo wa Gemini anasema kuwa ni kawaida kuingiza kiasi cha Dola za Kimarekani 500 kwa kazi ya sekunde tatu tu.

TRT Afrika