Kagame achaguliwa tena kuwa mwenyekiti wa chama tawala

Kagame achaguliwa tena kuwa mwenyekiti wa chama tawala

Uchaguzi mkuu ujao wa Rwanda utakuwa mwaka 2024.
Rwandan President Paul Kagame speaks during Armed Forces Day celebrations in Pemba / Photo: Reuters

Coletta Wanjohi

Rais wa Rwanda Paul Kagame amechaguliwa tena kuwa mwenyekiti wa chama tawala cha Rwanda Patriotic Front. Atahudumu kwa muhula mwingine wa miaka mitano katika nafasi hiyo.

Kagame alishindana na Abdul Karim Harerimana, ambaye alitangaza kuwania nafasi hiyo. Alipata kura 2,099 kati ya wapiga kura 2,102 huku mpinzani wake Harerimana akipata kura 3 pekee.

“Tumetimiza zaidi ya tulivyo feli. Kwa hiyo, lazima tubaki imara katika mtazamo wetu,” Kagame aliuambia mkutano mkuu wa 16 wa RPF.

Chama tawala pia, kwa mara ya kwanza kilimchagua mwanamke kama makamu mwenyekiti.

Uchaguzi mkuu ujao wa Rwanda utakuwa mwaka 2024.

Mrengo wa kijeshi wa Rwandan Patriotic Front unasifiwa kwa kukomesha mauaji ya halaiki ya 1994 ambayo yaligharimu maisha ya watu wapatao milioni 1.

RPF imetawala Rwanda chini ya Paul Kagame tangu wakati huo.

W

TRT Afrika