Serikali ya Rwanda imeondoa malipo ya ada katika angalau huduma kumi za serikali kwa umma.
Hii ni pamoja na uhamisho wa mali, kibali cha ujenzi katika mazingira ya vijijini na vyeti vya kuzaliwa.
Uhamisho wa umiliki wa nyumba na ardhi ni miongoni mwa huduma ambazo hazitavutia ada yoyote, kulingana na notisi ya Gazeti la Serikali iliyotiwa saini na rais Paul Kagame mnamo Desemba 4.
Usajili wa ardhi, idhini ya kukarabati jengo, idhini ya kuweka uzio kuzunguka jengo, kujenga nyumba kijijini, cheti cha kifo, idhini ya kuzalisha mkaa na matofali ya udongo, idhini ya uvunaji wa misitu, na maombi ya cheti cha ulezi hayatavutia ada zozote chini ya mwongozo mpya.
Kagame alisema kuwa wanaohitaji huduma hizo lazima, hata hivyo, waziombe kutoka kwa mamlaka husika.
Ada za zamani
Hapo awali, waombaji walilipa $16 kwa uhamisho wa umiliki wa mali, $4 kwa idhini ya kujenga vijijini, $1.60 kwa cheti cha ulezi, na faranga 1,200 ($0.96) kwa cheti cha kifo.
Huduma nyengine hapo awali zilitozwa kati ya $0.96 na $4.
Agizo hili la huduma bila malipo tayari limeanza kutumika.