Baraza la Haki za Binadamu limepitisha azimio la kusajili ukiukaji wa haki za binadamau nchini Sudan.
Katika mkutano wake Ijumaa baraza hilo liliuliza mtaalamu mteule wa Umoja wa Mataifa wa haki za binadamu nchini Sudan kurekodi madai yote ya ukiukaji wa haki za binadamu tangu tarehe 25 Oktoba 2021, ikiwa ni pamoja na yale yanayotokana na mzozo wa sasa.
Vita kati ya jeshi la Sudan na vikosi vya Rapid suport Forces vilianza mnamo tarehe 15 Mezi Aprili mwaka huu, na tayari imeanza kusababisha madhara makubwa ya kibinadamu.
Siku ya Ijiumaa pande hizi mbili zilitia saini makubaliano ya kusitisha vita kwasababu za kuwezesha majitahi ya kibinadamu kufikia wananchi .
Hata hivyo tayari vita vimeripotiwa kuendelea tena.
“Umoja wa Mataifa hautaacha juhudi zozote kusaidia katika utekelezaji wa azimio hilo na utaendelea kutoa misaada ya kibinadamu, ikiwa mapigano yatasitishwa au la,” mkurugenzi mkuu Antonio Guterres amesema katika taarifa.
“Wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu, wanaendelea kutoa msaada katika mazingira magumu sana nchini Sudan,” taarifa yake imeongezea.
Vita hivi vimepelekea wananchi wengi kukimbia katika nchi jirani za Misri. Chad, Ethiopia na Sudan Kusini.