Uchumi wa Kenya uliongezeka kwa asilimia 4.6 mwaka baada ya mwaka katika robo ya pili ya 2024, kutoka asilimia 5.6 katika robo inayolingana ya mwaka uliopita, ofisi ya taifa ya takwimu ilisema Jumatano.
Kwa mujibu wa data za benki Kuu, Robo ya pili ya 2023 data ya pato la taifa iliongezwa kutoka takwimu ya awali ya 5.0%.
Ofisi ya takwimu ya Kenya ilihusisha ukuaji wa robo ya pili na utendaji thabiti wa sekta zikiwemo kilimo, misitu na uvuvi, mali isiyohamishika, shughuli za kifedha na bima, na uuzaji wa jumla na rejareja.
Hata hivyo, sekta ya madini, uchimbaji mawe na ujenzi iliona mdororo, ofisi ya takwimu ilisema katika taarifa yake.
Wizara ya fedha ya Kenya imekadiria ukuaji wa uchumi wa 5.2% kwa 2024, kupungua kidogo kutoka 5.6% mwaka uliopita.
Kiwango cha mikopo
Wakati huo huo, Benki kuu ya Kenya imetakiwa kuzingatia kupunguza kiwango cha mikopo, ili kuimarisha ukopaji na ukuaji wa sekta binafsi.
Waziri wa Fedha wa Kenya John Mbadi, anasema kuwa hii imetokana na kupungua kwa mfumko wa bei katika miezi miwili iliyopita.
"Kiwango cha mfumuko wa bei kiko chini ya udhibiti sasa," Mbadi alisema wakati wa kufika katika Seneti.
Mfumuko wa bei ulishuka hadi 3.6% mwaka hadi mwaka Septemba kutoka 4.4% mwezi uliopita, wakati ulisimama kwa 4.3% mwezi Julai.
Serikali ya Kenya ilikuwa inalenga kiwango cha mfumuko wa bei cha kati ya 2.5% na 7.5% katika muda wa kati.
"Tunafikiri sasa benki kuu ianze kupunguza kiwango cha riba ili tuhamasishe sekta binafsi kuchukua mikopo zaidi, kutengeneza nafasi za kazi."
Benki kuu inatazamiwa kutangaza uamuzi wake ujao wa viwango vya riba tarehe 8 Oktoba.