Kenya economy

Uchumi wa Kenya ulikua kwa asilimia 5.6 mwaka 2023 kutoka asilimia 4.9 iliyofanyiwa marekebisho mwaka uliopita, mkuu wa ofisi ya takwimu alisema Jumatatu, akichochewa na pato thabiti katika sekta ya kilimo.

Uchumi wa taifa hilo la Afrika Mashariki unategemea kilimo ambacho kinachangia zaidi ya theluthi moja ya pato la uchumi la mwaka, na mvua nyingi baada ya ukame wa miaka mingi zilisaidia sekta hiyo kujikwamua kutokana na mdororo katika miaka miwili iliyopita.

Ukuaji ulirekodiwa katika sekta ya majani chai ambapo uzalishaji uliongezeka kutoka Ksh 156.7 bilioni mwaka wa 2022 hadi Ksh 176.3 bilioni mwaka wa 2023.

Uzalishaji wa mahindi kwa upande mwingine ulipanda hadi Shilingi Bilioni 11.3 kutoka B 7.9 huku uzalishaji wa miwa na maziwa ukipanda hadi Ksh B 34.1 na B 41 mtawalia. Hata hivyo, kahawa ilishuka kwa Ksh B 7.4 hadi Ksh B19.9.

Sekta ya kilimo inasemekana kupata ukuaji mkubwa kutokana na mvua kubwa iliyonyesha na ruzuku ya serikali kwa mbolea na vifaa vya kilimo.

Katika kipindi hicho, usawa wa kibiashara wa Kenya ulijiinua hadi Ksh 1.6 trilioni baada ya mauzo ya nje kuongezeka kwa 15.4pc kufikia kiwango cha juu cha kihistoria cha Ksh 1 trilioni kutoka Ksh 873.1 bilioni mwaka wa 2022, huku uagizaji uliongezeka kwa 4.9pc hadi Ksh 2.6 trilioni kutoka Ksh 2.5 trilioni.

Ongezeko hilo la mauzo ya nje lilichangiwa na chai iliyoipatia nchi Ksh 188.7 bilioni ikifuatiwa na kilimo cha bustani na mauzo ya nje ya thamani ya Ksh 187.4 bilioni.

Nchi inayoongoza kwa kununua bidhaa kutoka Kenya ni Uganda ambayo ilinunua bidhaa za thamani ya Ksh 126.3 bilioni ikifuatiwa na Pakistan yenye Ksh 78.9 bilioni.

Nchi hiyo pia ilisafirisha bidhaa za thamani ya Ksh 76.3 bilioni kwa Uholanzi, Ksh 69.3 bilioni kwa Tanzania na Ksh 64.3 bilioni kwa Marekani.

Mnamo 2023, Uchina ilikuwa nchi inayoongoza kwa uuzaji wa bidhaa zake Kenya kwa thamani ya Ksh 459 bilioni ikifuatiwa na UAE kwa Ksh 411 bilioni, India 269.2 bilioni, Saudi Arabia 145.2 bilioni na Malaysia Ksh 120.5 bilioni za uagizaji.

Pata habari zaidi kupitia Whatsapp channels

TRT Afrika