Kuelekea uchaguzi wa DRC Disemba 20, raia wa nchi hiyo wakiendelea na majukumu yao ya kila siku. Wengi wameiambia TRT Afrika, hamu yao ya kuona uchaguzi ukifanyika kwa amani na uhuru, huku wakisisitiza kwa yeyote atakae ingia madarakani kuhakikisha ana tatua changamoto za nchi ikiwemo kudumisha hali ya usalama hasa mashariki mwa nchi hiyo. Umoja wa Mataifa umeahidi kuisaidia Tume ya Uchaguzi nchini humo kusambaza baadhi ya vifaa vya kupigia kura katika baadhi ya maeneo ya nchi.  Picha/TRT Afrika. 
Kuelekea uchaguzi wa DRC Disemba 20, shughuli za kutafuta kipato zinaendelea mjini Kinshasa na katika maeneo mengine ya nchi. Vimesalia siku mbili kabla uchaguzi mkuu wa Disemba, 20.   DRC ni miongoni mwa nchi tajiri barani Afrika kutokana na rasimili zilizopo nchini humo. Hata hivyo, nchi hiyo kwa miongo kadhaa imekuwa ikikabiliwa na tatizo la usalama hasa mashariki mwa nchi. Picha/TRT Afrika.
Kuelekea uchaguzi wa DRC Disemba 20, katika kukabiliana na hali ya joto la Kinshasa wachuuzi wa maji wakiwa katika soko maarufu la Zando, lililopo jijini humo. Picha/TRT Afrika.   
Kuelekea uchaguzi wa DRC Disemba 20, mmoja wa wanawake wafanyabiashara katika jiji la Kinshasa wanaofanya biashara ya kuuza chakula akiwa katika sehemu yake ya kazi. Mama huyu aliyenaswa na kamera ya TRT Afrika, anasema amejiandaa kupiga kura siku ya uchaguzi. Katika uchaguzi huu, mwenye wagombea urais 22, kati ya hao, wawili ni wanawake.  Picha/TRT Afrika. 
Baadhi ya vijana wakiwa katika kampeni mjini Kinshasa nchini DRC. Zaidi wa wapiga kura milioni 40 wanatakiwa kujitokeza Disemba, 20 kuchagua viongozi wao kuanzia ngazi ya urais, ubunge na udiwani. Kampeni zimepamba moto, huku zikisalia siku mbili tu kabla ya uchaguzi huo kufanyika. 

Tume Huru ya Uchaguzi nchini DRC imesema, licha ya changamoto zilizopo hasa katika ushambazaji wa vifaa vya kupigia kura katika baadhi ya maeneo, lakini tarehe ya uchaguzi haitabadilika.

TRT Afrika