Kama ilivyotangazwa, treni inatarajiwa kuchukua dakika 90 kufika Morogoro. Tiketi ya kawaida kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro ni Sh13,000 kwa watu wazima na Sh6,500 kwa watoto wenye umri kati ya miaka 4 na 12.

"Hii ni hatua kubwa katika miundombinu ya usafiri ya Tanzania inayotarajia kuboresha uunganishaji na ufanisi na kuchochea ukuaji wa uchumi," alisema Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli la Tanzania, Masanja Kadogosa.

Naibu Waziri wa Uchukuzi David Kihenzile alisema abiria 1,400 kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro walisafiri katika treni ya kwanza ya umeme ya SGR bila malipo, na kuongeza kuwa treni iliondoka Dar es Salaam saa 12:10 asubuhi na kufika Morogoro saa 1:55 asubuhi.

"Shughuli za kibiashara za kwanza za umeme za SGR kati ya maeneo hayo mawili zilikuwa za kihistoria," alisema Kihenzile, na kuongeza kuwa nauli za kutoka na kurudi Dar es Salaam zililipwa na Rais Samia Suluhu Hassan kama shukrani yake kwa uzinduzi wa shughuli za kibiashara.

Kadogosa alisema mradi mzima wa SGR utakuwa na urefu wa kilomita 1,596, ukiwa na sehemu tano, kutoka Dar es Salaam hadi mkoa wa Mwanza.

Kulingana na Kadogosa, kasi iliyoongezwa ya treni itapunguza kwa kiasi kikubwa muda wa safari na kuwezesha usafirishaji mzuri wa bidhaa na watu kote Tanzania.

Mara itakapozinduliwa kikamilifu Julai 2024, treni za SGR, zikiwa na kasi ya wastani ya kilomita 160 kwa saa, zitapunguza muda wa safari kati ya Dar es Salaam na Morogoro hadi takriban saa mbili kutoka safari ya sasa ya saa nne kwa mabasi na saa tano kwa treni kwenye reli ya zamani ya kiwango cha mita, alisema.

Kama ilivyotangazwa, treni inatarajiwa kuchukua dakika 90 kufika Morogoro.

Tiketi ya kawaida kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro ni Sh13,000 kwa watu wazima na Sh6,500 kwa watoto wenye umri kati ya miaka 4 na 12.

TRT Afrika