Kenya, Rwanda, Burundi, Tanzania sasa zinaruhusu usafiri bila Viza kwa raia wa Congo. Zimesalia Uganda na Sudan Kusini pekee/ Picha TRT Afrika

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imefanya marekebisho ya Sheria yake ya Kanuni za Uhamiaji namba 54 na kuijumuisha Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo miongoni mwa nchi ambazo raia wake hawahitaji viza (visa-bure) kuingia nchini Tanzania. ", imesema taarifa kutoka kwa Ubalozi wa Tanzania nchini DRC, ambayo TRT Afrika iliweza kupokea nakala yake.

Tangazo hilo linakuja siku chache baada ya Kenya, nchi nyingine ya Afrika Mashariki, kufuta viza kwa raia wa Kongo.

Maamuzi yalipongezwa nchini DR Congo, haswa na raia kutoka Mashariki mwa nchi ambao wanadumisha uhusiano wa karibu sana wa kibiashara na Mataifa hayo mawili.

Hatua hii inakuja ili kukidhi matakwa ya Wakongomani ya uhuru wa kutembea kwa nchi hizi tangu DRC ilipojiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Aprili 8, 2022.

Raia wa  DR Congo, haswa kutoka Mashariki mwa nchi ambao wanadumisha uhusiano wa karibu sana wa kibiashara na Mataifa hayo mawili wamepokea habari hii kwa shangwe. / Picha : Ikulu DRC 

Kwa kujiunga na shirika hili la Afrika Mashariki, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ilipaswa kufaidika na msamaha wa visa kwa raia wake wanaotaka kwenda katika nchi zingine za jumuiya hiyo pamoja na manufaa mengine, hasa katika eneo la kodi na ushuru wa forodha.

TRT Afrika iliweza kuwasiliana na baadhi ya wafanyabiashara wa Kongo wanaotembelea nchi za Afrika Mashariki… Wanahisi kufarijiwa sana na hatua hizi kutoka nchi mbili.

"Nimefurahi ninaposoma, kupitia mitandao ya kijamii, taarifa za msamaha wa viza kwa Wakongo nchini Kenya na Tanzania... Hapo awali, nililipa dola 50 za Marekani kuingia Kenya na Tanzania. Hatua hii ni afueni kwetu," alisema Hassan Sadiki. , mfanyabiashara kutoka mji wa Beni mashariki mwa Kongo.

''Nchi za EAC zinaiona DRC kuwa soko kubwa la kuuza bidhaa zao na vile vile wao kununua kutoka huko.'' William Ruto kutoka Kenya na Samia Suluhu kutoka Tanzania walikuwa wameeleza haya hapo awali.

Hatua hii imeziacha Uganda na Sudan Kusini, nchi mbili za jumuiya ya Afrika Mashariki ambazo bado hazijafungua milango kwa raia wa Kongo, bila viza.

Rwanda na Burundi tayari walikuwa na viza huru kati yao na DRC tangu kitambo.

Ili kuingia Uganda, Wakongo lazima walipe $50 kupata visa ya kukaa kwa miezi mitatu, bila kujumuisha ada ya kipimo cha Covid-19, ambayo bado inatumika, ambayo ni $45.

TRT Afrika