Serikali ya Tanzania inalenga kuongeza gharama za ulinzi kwa asilimia 11.2, ikiwa ni sehemu ya kuboresha uwezo wa jeshi lake kupitia vifaa na nyenzo za kisasa.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa wa Tanzania Dkt Stergomena Tax ameliomba bunge la nchi hiyo kuidhinisha bajeti ya dola bilioni 22.7 kwa ajili ya Jeshi la Ulinza la Nchi hiyo (JWTZ) katika mwaka wa fedha 2024/25.
Kulingana na Tax, fedha hizo zitatumika kununulia vifaa vya kisasa vya kijeshi, mavazi pamoja na mazoezi.
“Tutaendelea kutengeza mazingira mazuri ya kufanya kazi kwa ajili ya majeshi yetu, ikiwemo makazi na huduma za afya,” alisema Dkt Tax, wakati wa hutoba yake kwa bunge hilo.
Pamoja na ulinzi wa mipaka ya nchi, Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania pia linaendelea na majukumu ya ulinzi wa amani sehemu mbalimbali zenye migogoro ndani na nje ya Bara la Afrika chini ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika.
Operesheni hizo ni pamoja na ECOMOG nchini Liberia, UNAMID huko Darfur, Sudan, UNIFIL nchini Lebanon na MONUSCO nchini DRC.