Nembo ya Kampuni ya Johnson & Johson./Picha: TRT Afrika.

Msemaji wa TMDA Gaudensia Simwanza aliiambia Reuters siku ya Jumatatu kuwa mamlaka hiyo imeanza kuondoa dawa hizo kuanzia tarehe 12 Aprili, kufuatia taarifa za vipimo kutoka Nigeria."

Hili ni zoezi ambalo halihusishi uchunguzi bali ufuatiliaji ili kuhakikisha kuwa dawa zenye athari kwa matumizi ya binadamu zimeondolewa sokoni," Simwanza amesema.

Tanzania inajiunga na Rwanda katika zoezi hilo la kuondoa dawa hizo katika soko.

Nchi hizo mbili, pia zinaungana na Nigeria, Kenya na Afrika Kusini kutekeleza azma hiyo ya kuondoa dawa hizo zenye kutibu kikohozi, homa na mzio kwa watoto.

Mdhibiti wa afya wa Nigeria alisema kuwa vipimo vya maabara vilivyo fanyika kwenye dawa hiyo vilionesha uwepo wa kiwango cha juu cha diethylene glycol, ambacho kimehusishwa na vifo vya makumi ya watoto nchini Gambia, Uzbekistan na Cameroon tangu 2022 katika moja ya milipuko mibaya zaidi ya sumu kusababishwa na dawa za kumeza duniani.

Reuters