Juhudi za kuwasaidia wahanga wa mafuriko na maporomoko ya ardhi wa Hanang, mkoani Manyara zimepata jeki leo kwa mchango wa shilingi Bilioni mbili zilizokabikdhiwa rais Samia Suluhu Hassan.
Hundi hiyo ilitolewa katika hafla Jumapili mchana katika ikulu ya Chamwino, kutoka kwa msajili wa Hazina Bw Nehemia Mchechu kwa niaba ya taasisi mbali mbali za serikali.
''Lengo la kuwachangia waathirika hao ni kuweza kuwapatia mahitaji muhimu ili waweza kurejea katika maisha yao ya kawaida,'' alisema Rais Samia katikataarifa kwa vyombo vya habari.
Vile vile Rais Samia ameitisha tathmini kamili kutoka ofisi ya Waziri Mkuu ya maafa hayo kwa waathirika ili serikali ianze mchakato wa kuwarejesha katika makazi rasmi
Katika taarifa yake, Rais Samia amewataka Watanzania wawe wazingatifu zaidi kwa mazingira kwa usalama wao.
''Tunawaomba wananchi kutunza mazingira kwa kusafisha na kuacha kutupa takataka katika mitaro, na kuhakikisha inazibuliwa kwa wakati ili kunaponyesha maji yaweze kutiririka kwa wepesi,'' aliongeza Rais Samia.
Zaidi ya watu 80 wamefariki katika mkasa mbaya wa mafuriko yaliyosababisha maporomoko ya ardhi katika mkoa wa Manyara Kaskazini mwa Tanzania.
Rais Samia Suluhu ambaye alikuwa akishiriki Mkutano wa kimataifa wa Mabadiliko ya Tabia nchi (COP28), uliokuwa ukifanyika Dubai, alilazimika kurejea nchini kuongoza juhudi za serikali za kukabiliana na athari za mafuriko hayo.
Serikali ya pia ilitangza kugharamia mazishi ya waliofariki katika mkasa huo pampoja na gharama za matibabu kwa wote wlaiojeruhiwa.
katika hatua za kuepusha kutokea janga kama hilo mkoani humo, Rais aliwaagiza wananchi wanaishi au kuendesha shughuli za kibiashara karibu na mto Jorodom kuhamishwa zaidi ya mita 300 mbali na kingo zake.