Rais Samia alitoa tamko hilo jana katika kongamano la wanawake wa Kiislam Zanzibar mwezi 27 katika maadhimisho ya mwaka mpya wa Kiislamu 1445 – Hijjiria.
Aidha, Rais Samia amesema kila mwanamke ana wajibu wa kusimamia maadili kwa kuwa ana mchango mkubwa sana katika kujenga au kumomonyoa maadili ya familia na jamii kwa ujumla.
Vile vile, Rais alisema hivi sasa wanawake wamekuwa mstari wa mbele kupigania haki na kushiriki katika masuala ya kitaifa na kijamii kwa kufanya kazi kwa uadilifu, uhakika na weledi mkubwa ambazo awali walidhaniwa hawaziwezi.
Kupitia taarifa kwa vyombo vya habari kutoka Ikulu rais Samia amewataka wanawake kujiepusha na vitendo vya unyanyasaji kwa kuwa vinarejesha nyuma maendeleo ya kiuchumi, kisiasa na kijamii.
Rais Samia pia amesema ukosefu wa elimu ya msingi ya dini unaathiri jamii na kusababisha vitendo vinavyokiuka maadili kama udhalilishwaji wa kijinsia, wizi na matumizi ya dawa za kulevya na kuliondoshea taifa heshima, haiba na kuua vizazi vyetu.