Tanzania kupitia mamlaka yake usambazaji umeme, Tanesco, imesema inatarajia kueneza vituo vya kuchaji magari ya umeme nchini humo ifikapo 2024 pale ambapo huduma hiyo itahitajika.
"TANESCO ina mpango kwa kununua magari ya umeme na kutumia kwenye kazi zetu mijini.", wasema Tanesco kupitia maongezi na TRT Afrika.
Vituo zaidi vya kuchaji pamoja na gharama za chini za uendeshaji vinarahisisha kuachana na uchafuzi wa mazingira ya magari ya petroli. Magari ya umeme, EVs, yanazidi kushika kasi duniani kote huku makampuni ya kielektroniki yakianzisha njia za kuchaji betri. Kuchaji kwa umeme hupunguza utoaji wa kaboni, muhimu katika vita dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa.
Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa, UNDP, uliweka kituo cha kwanza cha kuchajia magari ya umeme nchini Tanzania katika mji mkuu huko Dodoma, kwa ushirikiano na Wizara ya Nishati na Madini kama ilivyochapishwa kwenye ukurasa wake wa Twitter tarehe 4 Mei.
"Habari za kusisimua! Tunaweka kituo cha kwanza cha kuchaji magari ya umeme Dodoma 🇹🇿! Hili ni hatua kubwa kwa malengo ya hali ya hewa ya nchi yetu, na tunajivunia kuongoza njia kuelekea zaidi" UNDP ilichapisha mtandaoni
"UNDP inaunga mkono Wizara ya Nishati katika kutekeleza mpango kazi wa kwanza wa ufanisi wa nishati nchini Tanzania kwa msaada wa EU. Madhumuni ya jumla ya mradi ni kuhakikisha upatikanaji wa nishati nafuu, ya kutegemewa, endelevu na ya kisasa kwa wote nchini Tanzania.” Aaron Cunningham, Meneja Mradi wa UNDP, Mradi wa Ufanisi wa Nishati katika mahojiano na TRT Afrika.
Hata hivyo hakuna magari ya umeme ya kuzungumzia kwa sasa Dodoma. Usafiri unaopendelewa na maafisa wakuu wa serikali na wabunge nchini Tanzania bado ni Toyota Land Cruiser inayotumia dizeli au petroli.
"Kama unavyofahamu mradi wetu mkubwa wa Julius Nyerere uko katika hatua za mwisho na mwakani mwezi wa Sita (Juni) tunategemea kuanza kuwasha Mtambo mmoja; hivyo tuna uhakika wa kuwa na uwezo wa kuwahudumia watumiaji wa magari ya Umeme." Tanesco inasema.
Mradi wa bwawa la Julius Nyerere unatarajiwa kuongeza Megawati 2115 ya umeme katika gridi ya taifa.
Megawati moja katika saa moja ni sawa na kiasi cha umeme kinachotumiwa na nyumba 350 kwa saa.
Kupunguza alama ya kaboni
"Mradi huu unahusisha kubadilisha injini za mwako za ndani (ICE) na Magari ya Umeme, yani EVs." Kulingana na Cunningham, akiongeza kuwa kwa kutumika kama mpango mkali, mradi huu unalenga kuangazia faida za EVs na kuongeza ufahamu wa wananchi juu ya jukumu lao muhimu katika "kuunda mustakabali endelevu."
Mjasiriamali kutoka Tanzania na Mtangazaji wa Redio, Masoud Kipanya alitambulisha gari ambalo ni rafiki kwa mazingira, lililopewa jina la Kaypee, ambalo limetengenezwa kwa vifaa vya asili. Hili lilipokelewa vyema na kuungwa mkono na serikali ya Tanzania. Sasa kutakuwa na mahali pa gari la umeme la aina hilo kuegesha na kuchaji mara kwa mara.
"Utoaji wa vituo vya kuchajia magari ya umeme bado uko katika hatua za awali duniani kote, kwani magari mengi barabarani yanaendelea kuendeshwa na injini za mwako za ndani. Walakini, mwelekeo unaelekea kupitishwa kwa EVs katika masoko mengine mengi." Anaeleza Cunningham.
Nchini Tanzania, sio tofauti, mradi huu unahakikisha kwamba ingawa haya ni maonyesho ya majaribio, wanatamani kuona uwekaji wa vituo vingi vya kuchaji vya EV kote nchini, wakati dunia inaelekea kwenye nishati safi na kupunguza uzalishaji wa gesi chafuzi.
Katika maongezi maalum na TRT Afrika, Tanesco wameeleza kuwa "kama UN wata fanya mradi itaongeza uraisi kwa TANESCO na pia kwa kua TANESCO ndio muuzaji wa umeme basi TANESCO inategemea biashara kutokana na matumizi ya EVs huko mbeleni."
Umoja wa Ulaya, EU, ilipitisha sheria mwaka jana ambayo itahitaji magari yote mapya yanayouzwa katika umoja wa ulaya kuwa na hewa sifuri ya CO2 kutoka 2035.
Hii inaweza kuwa na athari kwenye masoko mengine. "EVs ndiyo teknolojia ya mbeleni, kwa hivyo wakati wa kujiandaa ni sasa." Aliongeza Cunningham.
Swali linabaki kuwa iwapo ujenzi wa vituo vya kuchaji vya EV unaofanya, katika nchi ambayo bado ni changa katika matumizi ya magari yanayo tumia umeme, unaweza kuihamasisha Tanzania kubadilisha mfumo wake wa sasa ikizingatiwa kuwa gari la kawaida huchukua saa 8 -10 kujaa chaji.
Athari Ulimwenguni
Tanzania iliazimia kuchukua hatua za dharura kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi na Mpito wa Nishati wakati wa COP27 nchini Misri mwaka jana. Ili kupunguza utoaji wa gesi chafuzi na kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa, kumekuwa na mwelekeo wa kimataifa kuelekea ufumbuzi endelevu katika nyanja mbalimbali, ikiwa ni pamoja na usafiri.
Tanzania imechelewa kidogo, wenzao wa Kenya wamepata vituo vyao vya kuchaji vya Kengen mwaka jana Julai na Uganda ilipata vituo vya kuchaji mabasi ya umeme mnamo Agosti tusije tukasahau Rwanda pia ilizindua mapema 2023.
Kama sehemu ya maonyesho ya malengo ya kimataifa, Tanzania kupitia UNDP pia imeweka Solar PV, ambayo itaendesha ofisi na kuchaji magari mapya ya umeme. Mitambo ya jua na EV zote zitachangia katika kupunguza uchafu wa hewa ukaa na kuufanya mji wa Dodoma kuwa wa kijani kama ilivyopangwa pia na Rais wa nchi Samia Suluhu Hassan.