Mradi wa mradi wa kufua umeme wa Julius Nyerere nchini Tanzania umefikia asilimia 99, Serikali ya nchi hiyo imesema.
Katika mahojiano na TRT Afrika, Naibu Waziri wa Nishati wa Tanzania Judith Kapinga amesema kuwa mradi huo unaogharimu zaidi ya trilioni Dola Bilioni 2.2 (Trilioni 6.5 za Kitanzania), umefikia hatua ya kuridhisha, tayari kuzalisha megawati 705 kwenye Gridi ya Taifa.
"Mitambo mitatu tayari imeshawashwa, yenye uwezo wa kuzalisha megawati 235 kila mmoja, hivyo kuzalisha jumla ya megawati 705 zinazoingizwa katika gridi ya taifa," Waziri huyo amesema.
Kulingana na Kapinga, mradi huo ulianza kufanya kazi mwezi Februari 2024, baada ya kuwasha mtambo wa kwanza na kuingiza kiasi cha megawati 235 katika gridi ya taifa.
Mradi huo ukikamilika unatarajiwa kuzalishaji megawati 2,115 na kuifanya Tanzania yenye mahitaji ya Megawati 1,669.39 iwe na umeme wa kutosha.
Serikali ya nchi imeshamlipa mkandarasi kampuni ya JV Elsewedy na Arab Contractors shilingi Trilioni 6.17 ambayo ni sawa na asilimia 94.